Hatimae muvi
ya Kimondo na Yanga imefika mwisho baada ya katibu wa Yanga Jonas Tiboroha
kufunga safari na kwenda viunga vya Mbozi
kumalizana na Kimondo Sc.
Akizungumza
kwa njia ya simu kutoka Mbozi katibu wa
Yanga amesema tatizo lililokuwa kati ya pande hizo mbili limeisha .
“Tumekubaliana
mengi na Kimondo fc mengine hatuwezi
kuweka hadharani mojawapo likiwa ni pamoja na kuja kucheza na Kimondo fc na
mapato yote kwenda kwa Kimondo fc ikiwa ni sehemu ya shukrani kwa kumkuza
Mwashiuya mpaka Yanga tukamuona.”
“Yamesemwa
mengi sana na mengi yalikuwa ya uongo na ugovi ukatokea lakini Yanga tumetambua
kuwa mwashiuya ni tunda kutoka Kimondo ndio maana tumekuja lakini nataka kusema kama yanga tukitaka
mchezaji huwa hatumkosi kwa vyovyote vile kwa iyo tumemalizana na Kimondo na
Mwashiuya ataitumikia Yanga kuanzia leo.”
Kwa upande
wa msemaji wa Kimondo fc Chriss Kashililika naye amekiri kupokea uongozi wa Yanga na kumaliza
tatizo hilo.
“Kwa sasa
Mwashiuya ni mchezaji halali wa Yanga sisi kama Kimondo tumekubali Yanga
wamekubali kuwa Mwashiuya ni mchezaji wa Kimondo ndio maana Yanga wamemtuma
katibu mkuu kuja kulimaliza hili .”
Sisi Kimondo
tunawajulisha umma kuwa kuanzia leo Mwashiuya ni mchezaji halali wa Yanga baada
ya kumalizana na Yanga tumekubaliana mengi ikiwemo na Yanga kuja kucheza mechi
Mbozi alikotokea Mwashiuya na Yanga wamekubali watacheza watapokuja kwenye ligi
.”
Makubaliano yote yapo kwenye maandishi kama itatokea Kimondo watakuwa nje basi Yanga
watakuja kwa mara nyingine lakini pia Yanga wamemuomba radhi mkurugenzi wa
kimondo Eliki Ambakisye kwa yale maneno
ya fedheha aliyoongea Jerry Murro.
No comments:
Post a Comment