Siku chache zilizopita, msanii wa muziki wa HipHop Marekani, Tyga aliingia kwenye headlines baada ya taarifa kusambaa kuwa yeye na mpenzi wake wa miaka 18,Kylie Jenner wameachana
Hiyo ilikuwa wiki iliyopita, ila jana Kylie Jenner alizitembelea TV Studios za Ellen Degeneres kwa ajili ya kufanya nae interview na akiwa huko, model huyo alikiambia kipindi hicho cha TV kuwa yeye na Tyga bado wapo pamoja!
>>> “Hatujaachana, kusema kweli watu wameichukulia hii ndivyo sivyo… hatujaachana. Tulikuwa mabesti hata kabla ya kitu chochote kutokea kati yetu, mimi nadhani hiko ni kitu poa sana, tunapenda kuspend time pamoja“. <<< Kylie Jenner.
‘Kuspend time pamoja?!’… jibu hili halikumkaa sawa Ellen, na alipomuuliza model huyo ‘kuspend time pamoja’ inamaanisha nini, Kylie Jenner alicheka na kusema… “Bado tupo pamoja”… Ellen akaendelea kugusia kuhusu Ferrari aliyozawadiwa na Tyga siku ya birthday yake, jibu la Kylie lilikuwa… “Najua, ndilo nililoliendesha kuja hapa”.
No comments:
Post a Comment