Monday 18 January 2016
AC Milan Yampeleka Mahakamani Mchezaji Huyu Kutoka Afrika Kwa Kosa La Kudanganya Umri
Wachezaji wa Africa mara nyingi huwa wanajikuta kwenye tatizo la kudanganya umri wakiwa wanataka kucheza Ulaya, Yusupha Yaffa ni mchezaji wa Gambia ambae alifanikiwa kuiongopea club kubwa AC Milan kwamba ana miaka 19 wakati ana miaka 28.
Mchezaji huyu alifanikiwa kuingia kwenye mpango wa timu ya vijana na kucheza kwenye kikosi cha u19 baada ya viongozi wa club hiyo kukubali ana miaka 19.
Taarifa za mchezaji huyu kugundulika kwamba ana miaka 28 na sio 19 ilianzia kwenye Facebook ambapo rafiki yake aliweka post ambayo inaelezea ishu hiyo.
Sasa hivi mchezaji huyu anacheza nchini Ujerumani club ya MSV Duisburg na huko pia inasemekana mkataba unakaribia kuvunjwa kwasababu ya ishu hii.
AC Milan imefungua mashtaka ndani ya mahakama ya Italy dhidi ya mchezaji huyu. Hii sio mara ya kwanza kwa Yaffa kufikishwa mahakamani, aliwahi kuwa na kesi ya kumbaka binti mmoja huko Ujerumani.
Labels:
AddyTz
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment