Social Icons

Monday 18 January 2016

Taarifa Mbaya Juu Ya Mwandishi wa Kitabu Pendwa NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE Hii Hapa


Mwandishi maarufu wa tamthilia na kitabu cha ‘Ngoswe, Penzi Kitovu cha Uzembe’, Edwin Semzaba amefariki dunia , Semzaba ambaye kitabu chake cha Ngoswe, Penzi Kitovu cha Uzembe kilimpatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania, aliwahi kueleza kuwa alianza kuandika kitabu hicho akiwa anasoma kidato cha pili akiwa na umri wa miaka 16 tu.






Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe ni tamthilia ambayo imekuwa ikitumika katika mtaala wa kufundishia katika shule za sekondari nchini na kupendwa sana na wanafunzi kutokana na maudhui yaliyo ndani ya tamthilia hiyo.




Moja ya mambo ambayo yapo katika kitabu hicho ni pamoja na jinsi penzi lilimfanya Ngoswe kushindwa kufanya kazi ya serikali ya kuhesabu watu na kujikuta akiingia katika mapenzi na kusababisha kazi yake kuharibika.Semzaba pia aliandika tamthilia nyingine kama vile Kinyamkera, Joseph na Josephne, Mkokoteni na Sophia wa Gongo la Mboto. 

Mbali na kuwa mwandishi maarufu, Semzaba alikuwa mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Pia, alikuwa mwenyekiti wa Umoja Wa Waandishi wa Vitabu Tanzania (UWAVITA).

Hakika mchango wake utakumbukwa na wapenda tamthilia na watanzania kwa ujumla kwani mafundisho yake ndiyo maisha halisi katika jamii.

No comments:

Post a Comment