Manchester United wakicheza Uwanjani kwao Old Trafford wameifunga Everton Ba0 2-1 katika Mechi ya Ligi Kuu England huku Kipa wao David De Gea akiwa Shujaa kwa kuokoa Penati na Bao kadhaa lakini aliewapa ushindi ni Straika Radamel Falcao
aliefunga Bao la Pili na la ushindi na hilo ni Bao lake la kwanza kwa Man united.
Man United walipata Bao lao la kwanza Dakika ya 27, Angel Di Maria alipofunga Bao safi kufuatia Krosi ya Rafael kuokolewa na Jagielka na Mpira kumfikia Juan Mata aliemsogezea Di Maria na kufunga.
Dakika ya 47, baada ya Dakika 2 kuongezwa kwenye Kipindi cha Kwanza, Refa Kevin Friend aliwapa Everton Penati kwa madai Luke Shaw amemwangusha Tony Hibbert na Penati hiyo kupigwa na Leighton Baines ambae hadi sasa amefunga Penati 14 kati ya 14 alizopiga kwenye Ligi Kuu England lakini hii Leo alikosa baada Kipa David De Gea kuokoa vizuri.
Hadi Mapumziko Man United 1 Everton 0.
Everton walisawazisha Dakika ya 55 kwa Bao la Steven Naismith alipounganisha kwa Kichwa kufuatia Krosi ya Leighton Baines.
Dakika ya 62, Krosi ya Angel Di Maria iliunganishwa vizuri Radamel Falcao na kufunga Bao lake la kwanza kwa Man United na kuifanya Timu yakr iongoze 2-1.
Mwishoni mwa Mechi hii, Kipa wa Man United aligeuka shujaa kwa mara nyingine kwa kuokoa Bao 2 za wazi.
VIKOSI:
VIKOSI:
MAN UNITED: De Gea; Rafael, McNair, Rojo, Shaw; Blind; Valencia, Di Maria; Mata; Falcao, van Persie.
Akiba: Januzaj, Lindegaard, Fletcher, Fellaini, Thorpe, Blackett, Wilson
EVERTON: Howard, Hibbert, Jagielka (c), Stones, Baines, Barry, Besic, Pienaar, McGeady, Naismith, Lukaku
Akiba: Robles, Gibson, Eto'o, Oviedo, Osman, Browning, Alcaraz
REFA: Kevin Friend
MSIMAMO
NA
|
TIMU
|
P
|
GD
|
PTS
|
1
|
Chelsea
|
6
|
12
|
16
|
2
|
Man City
|
7
|
7
|
14
|
3
|
Southampton
|
6
|
7
|
13
|
4
|
Man United
|
7
|
3
|
11
|
5
|
Swansea
|
7
|
2
|
11
|
6
|
Arsenal
|
6
|
4
|
10
|
7
|
Liverpool
|
7
|
0
|
10
|
8
|
Aston Villa
|
7
|
-5
|
10
|
9
|
Hull
|
7
|
0
|
9
|
10
|
Leicester
|
7
|
-1
|
9
|
11
|
Sunderland
|
7
|
1
|
8
|
12
|
Tottenham
|
6
|
1
|
8
|
13
|
West Brom
|
7
|
-1
|
8
|
14
|
Crystal Palace
|
7
|
-2
|
8
|
15
|
Stoke
|
7
|
-2
|
8
|
16
|
West Ham
|
6
|
0
|
7
|
17
|
Everton
|
7
|
-3
|
6
|
18
|
Newcastle
|
7
|
-7
|
4
|
19
|
Burnley
|
7
|
-7
|
4
|
20
|
QPR
|
6
|
-9
|
4
|
No comments:
Post a Comment