Hii ni Mechi ambayo Manchester United wanataka kulipa kisasi kwa kufungwa na Everton Mechi zote mbili za Ligi Kuu England Msimu uliopita kitu ambacho huko nyuma kilikuwa adimu kutokea.
Hata hivyo Everton ni Timu ambayo chini ya Meneja Roberto Martinez imebadilika na kuwa ngangari na itabidi Kikosi cha Louis van Gaal kicheze kiume sana ili kupata ushindi hasa ukizingatie watamkosa Nahodha wao Wayne Rooney ambae ndie anaanza Kifungo chake cha Mechi 3 baada kulambwa Kadi Nyekundu Mechi iliyopita waliyoifunga West Ham 2-1.
Hali za Wachezaji
Man United
Jana Louis van Gaal amethibitisha Kinda wa Miaka 19 Paddy McNair ataanza kama Sentahafu kama alivyocheza Mechi iliyopita ambayo ilikuwa ni Mechi yake ya kwanza kabisa.
Pia Van Gaal alidokeza Juan Mata ataanza Mechi hii kuchukua nafasi ya Wayne Rooney.
Lakini Man United watawakosa Majeruhi Phil Jones, Ander Herrera, Chris Smalling na pia Marouane Fellaini na Michael Carrick ambao wameshapona lakini bado kuwa fiti kwa ajili ya Mechi.
Everton
Everton itamkosa Kevin Mirallas ambae ameumia Musuli za Pajani lakini kina Sylvain Distin, James McCarthy, Steven Pienaar na Seamus Coleman ambao hawakwenda Urusi kuiva FC Krasnodar Juzi Alhamisi Usiku kwenye Mechi ya Kundi lao la EUROPA LIGI wanatarajiwa kuwepo kwenye Mechi hii.
Uso kwa Uso
-Everton wameshinda Mechi 3 kati ya 4 walizocheza mwisho na Manchester United kwenye Ligi Kuu England.
-Uwanjani Old Trafford, Everton wameshinda Mechi 2 tu kati ya 22.
-Ikiwa Everton watashinda Mechi hii huu utakuwa ushindi wao wa 3 mfululizo dhidi ya Man United kitu ambacho hakijatokea tangu Mwaka 1921.
VIKOSI VINATARAJIWA:
Man United: Dea Gea, Rafael, Paddy MacNair, Marcos Rojo, Luke Shaw, Daley Blind.
Valencia, Juan Mata, Robin van Persie, Radamel Falcao, Angel Di Maria
Everton: Howard; Hibbert, Stones, Jagielka, Baines; McCarthy, Barry, Besic; Mirallas, Naismith, Lukaku.
REFA: Kevin Friend
Jumapili Oktoba 5
1400 Man United v Everton
1605 Chelsea v Arsenal
1605 Tottenham v Southampton
1815 West Ham v QPR
No comments:
Post a Comment