Viongozi wa Uchina wanasema kuwa maandamano ya kupigania haki ya kuimarisha demokrasia katika eneo la Hong Kong yataambulia patupu.Taariri yenye matamshi makali katika Gazeti la Kikomunisti ilikariri kuwa Serikali inaendelea kumuunga mkono Mkuu wa eneo la Hong Kong, CY Leung.
Tahariri hiyo ya the People's Daily ilisema kuwa Serikali Kuu ya Uchina haina nafasi ya kuafikiana na kundi lo lote la waandamanaji.
Gazeti hilo la kikomunisti ni la Serikali na taarifa linalotoa ndio msimamo rasmi wa Serikali.
Utawala wa Hong Kong umekubali kukutana na viongozi wa wanafunzi wanaopigania haki ya kuimarisha demokrasia katika eneo hilo ingawa Serikali ya Beijing kwa upande wake haijaonyesha ishara ya kulegeza msimamo wake mkali.
Tahariri hiyo ilisema kuwa uamuzi wa Serikali kuu wa kupiga msasa wagombezi wa viti mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2017 hautapingwa na ye yote.
Serikali ya Uchina inajaribu kadiri ya uwezo wake kujaribu kuzima habari juu ya maandamano yanayoendelea Hong Kong yasienezwe katika vyombo vya kitaifa katika Uchina Bara.
Katika mji mkuu wa Beijing, inadaiwa kuwa watu wanne waliodhaniwa kupanga mkutano wa wachoraji ili kuwaunga mkono wanaoandamana Hong Kong, wamezuiliwa Gerezani.
No comments:
Post a Comment