Fifa imetetea Adhabu zake ilizompa Straika wa Uruguay Luis Suarez kwa kumuuma Meno mpinzani Uwanjani lakini Nchi yake imekasirishwa na Kocha wao kuamua kujiuliza toka Jopo la Ufundi la FIFA.
Suarez amefungiwa na FIFA Miezi minne
kutojihusisha na chochote kuhusu Soka ikiwemo kutokanyaga Mazoezi na
kutoingia Uwanja wowote wa Mpira na pia kutocheza Mechi 9 za Kimataifa
za Uruguay pamoja na kupigwa Faini ya Dola 111,000.
Lakini Uruguay imedai Mchezaji wao
ameonewa na hilo limemfanya Kocha wao, Oscar Tabarez, kutangaza kujitoa
Jopo la Ufundi la FIFA la Makocha kwa madai hawezi kushirikiana na
Taasisi isiyokuwa na haki.Hata hivyo, Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke, amesema Adhabu ya Suarez ni sahihi na imezingatia makosa yake ya Siku za nyuma.
Suarez amewahi kufungiwa mara 2 kwa kosa hilo hilo la kung’ata Wachezaji wa Timu pinzani wakati wa Mechi.Jerome Valcke ameeleza: “Hii si mara ya
kwanza na ilibidi tutoe fundisho. Tukio lile limeonekana na Mamilioni ya
Watu Dunia nzima. Hilo halitakiwa kuonekana na Watoto Dunia nzima
wanaocheza Soka.”
Vile vile, Jerome Valcke amemtaka Suarez kutafuta ushauri wa Madaktari wa Saikolojia ili kumfanya asirudie tena kosa hilo.Kwenye Mahojiano na Wanahabri kuhusu
Mechi yao inayowakabili ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Kombe la Dunia
dhidi ya Colombia, Kocha wa Uruguay, Oscar Tabarez, alikataa kuongea
chochote na badala yake kusoma Taarifa ya Dakika 14.
Kwenye Taarifa hiyo, Tabarez amevilaumu
Vyombo vya Habari, na hasa vya Uingereza, kwa kuukuza mgogoro huo
kutomtakia mema Mchezaji wao.Jana Ijumaa, Suarez alirudishwa Nchini kwao Uruguay.
Mbali ya Adhabu, Suarez sasa pia
anakabiliwa na kuachwa na Wadhamini ambapo wengine wameshamtoa kwenye
udhamini huku Adidas ikitangaza kutomtumia katika Matangazo yao ya Kombe
la Dunia.
No comments:
Post a Comment