Kocha wa Brazil Luiz Felipe Scolari amesema Timu yake imebakisha Gemu 3 kufika ’Peponi’ baada Jana kuibwaga Chile kwa Mikwaju ya Penati 3-2 baada ya Sare ya Bao 1-1 katika Dakika 120 za Mchezo za Mechi ya Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia.
Kwenye Robo Fainali, Brazil watacheza na Colombia ambao Jana waliwafunga Uruguay 2-0.Scolari amesema: “Tuliazimia wenyewe
kwenye dhima hii tuwe Mabingwa. Ukiweka ahadi ni lazima uitimize. Hili
ndio Wachezaji wanafanya!”
Aliongeza: “Bado zipo Gemu 3 zaidi na tutaona kama tutafika peponi!”
Kabla ya Mechi na Chile, Scolari alikiri kucheza na Chile ni ‘maumivu’ na pia kubaini Wachezaji wake kidogo wana mchecheto.
Scolari, ambae aliiongoza Brazil kutwaa
Kombe la Dunia Mwaka 2002, alisema: “Kila Mechi inazidi kuwa ngumu na
ugumu unaongezeka! Kombe la Dunia limeonyesha Timu zinalingana. Kama
hutumii nafasi moja au mbili unazopata, kama tulivyofanya Leo, basi
unaweza kuadhirika na kutolewa.”
KOMBE LA DUNIA: COLOMBIA YAIPIGA URUGUAY, ROBO FAINALI KUIVAA BRAZIL!
James Rodriguez, Kijana wa Miaka 22 anaechezea AS Monaco ya Ufaransa, Jana alifunga Bao 2 na kuipeleka Colombia, kwa mara ya kwanza katika Historia yao, Robo Fainali ya Kombe la Dunia baada Colombia kufunga Uruguay Bao 2-0 Estadio Maracana Jijini Rio de Janeiro Nchini Brazil.
James Rodriguez pia ameweka Rekodi ya
kuwa Mchezaji wa kwanza tangu Ronaldo wa Brazil Mwaka 2002 kufunga Bao
katika kila Mechi katika Mechi zake 4 za kwanza za Fainali za Kombe la
Dunia.
Uruguay, wakicheza bila Staa wao Luis
Suarez aliefungishwa virago na FIFA kwa kufungiwa Miezi Minne kwa
kumng’ata Beki wa Italy Giorgio Chiellini, walizidiwa maarifa na Timu ya
Ciolombia Kwenye Robo Fainali, Colombia watacheza na Wenyezi Brazil hapo Ijumaa Julai 4 huko Estadio Estadio Castelão, Fortaleza.
No comments:
Post a Comment