Usalama umeimarishwa katika mji huo kufuatia shambulizi hilo lililowauwa watu 21 na kuwajeruhi wengine 52.
Hatua ya Bwana Johnathan kurudi inafuatia shtuma kwamba ameshindwa kukabiliana na ghasia nchini humo.Wapiganaji wa kundi la Boko haram wameimarisha mashambulizi yao nchini Nigeria.Mnamo mwezi Aprili,wapiganaji hao waliwauwa zaidi ya watu 70 katika mlupuko wa bomu katika kituo kimoja cha basi viungani mwa mji wa Abuja.
Kundi hilo pia limekiri kutekeleza shambulizi la bomu lililotegwa ndani ya gari karibu na kituo cha mabasi katika kijiji cha Nyanya mnamo mwezi May,ambalo liliwauwa watu 19 na kuwajeruhi wengine 60.
Msemaji wa rais Reuben Abati amesema kuwa Jonathan alipata habari kuhusu mlipuko huo wakati alipokuwa akiwasili katika hoteli yake katika mji wa Malabo nchini Equitorial Guinea alikoelekea kwa mkutano umoja wa afrika kulingana na gazeti la Premium Times nchini Nigeria.Aliamua kurudi nchini Nigeria ili kukabiliana na tatizo hilo,alisema bwana Abati.
Maafisa wa polisi wameagiza kuongezwa kwa usalama pamoja na uchunguzi ndani na hata viungani mwa mji wa Abuja ili kuepuka mashambulizi zaidi,alisema.
No comments:
Post a Comment