Kambi ya Brazil imechukizwa na kampeni
ya Chile ya kutaka kumpa presha Refa kutoka England, Howard Webb, ambae
ndie atakaechezesha pambano lao la Leo la Raundi ya Mtoano ya imu 16
huko Estadio Mineirao, rasmi kama Estádio Governador Magalhães Pinto,
Jijini Belo Horizonte.
Watu kadhaa wa Timu ya Chile, akiwemo Straika Alexis Sánchez, wamesema wana wasiwasi na uchezeshaji wa Marefa.
Mchecheto wao unakuja kufuatia madai ya
kichinchini kuwa Waamuzi wamekuwa wakiipendelea Brazil na kunyooshea
kidole Penati waliyopewa Brazil walipocheza na Croatia baada ya Fred
kuangushwa na pia Bao la Straika huyo huyo dhidi ya Cameroon kukubaliwa
kukiwa na madai ni Ofsaidi.
Chile pia walimlalamikia Refa kutoka
Gambia Bakary Gassama aliechezesha walipofungwa 2-0 na Holland kwenye
Mechi yao ya mwisho ya Kundi B Jumatatu iliyopita.Alexis Sanchez amesema: “Ninafurahi sana
kucheza dhidi ya Brazil lakini kitu kinachonipa wasiwasi mkubwa ni
uchezeshaji wa Marefa!”
Hii itakuwa mara ya pili mfululizo
Howard Webb kuichezesha Brazil na Chile kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu
16 ya Kombe la Dunia kwani Mwaka 2010 huko Afrika Kusini alichezesha
Mechi hii hii na Brazil kuinyuka Chile Bao 3-0 na kulikuwa hamna
manung’uniko yeyote.
Mwandishi wa Chile alijaribu kuliingiza
swali la Marefa kwenye Mahojiano ya Kocha wa Brazil, Luiz Felipe Scolari
akiwa na Nahodha wake Thiago Silva, na Wanahabari lakini Mkurugenzi wa
Mawasiliano wa Brazil, Rodrigo Paiva, aliingilia kati na kujibu:
“Tutaongelea hili mara moja tu. Wanahabari huko Chile wamesisitiza suala
hili Wiki yote sasa na hiki ni kitu hakistahili. Hii ni presha ya
kipuuzi.”
Aliongeza: “Kuongelea hili si kuvunja heshima kwa FIFA, kwa Refa au kwa Timu ya Taifa ya Brazil, ‘Selecao’
au Watu wanaofanya kazi hapa kwa bidii kubwa, kwa Nchi yenye Historia
ya Soka ya Miaka 100, Historia ya ushindi, hii ni kuvunjia heshima kwa
Watu wa Brazil. Brazil haihitaji Refa kushinda Mechi na lazima
uwaheshima ‘Selecao’ na Watu wa Brazil!’’
Uso kwa Uso
-Brazil na Chile zimekutana mara 68 na Brazil kushinda 48, Chile 7, Sare 13
-Brazil imeifunga Chile Bao 159-58
-Kwenye Kombe la Dunia, Raundi za
Mtoano, Brazil na Chile zimekutana mara 3 na zote Brazil kushinda. Mwaka
1962, kwenye Nusu Fainali, Brazil ilishinda 4-2. Mwaka 1998, Raundi ya
Mtoano ya Timu 16, Brazil walishinda 4-1 na huko Afrika Kusini, Mwaka
2010 pia Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Brazil ilishinda 3-0.
VIKOSI VINATARAJIWA:
Brazil: Cesar; Dani Alves, Thiago Silva, David Luiz, Marcelo; Paulinho, Luiz Gustavo; Willian, Oscar, Neymar; Fred
Chile: Bravo; Isla, Medel, Jara, Mena; Gutierrez, Aranguiz, Diaz, Valdivia; Sanchez, Vargas
REFA: Howard Webb [England]
No comments:
Post a Comment