Ripoti toka Ghana zimedai kuwa Rais wa Nchi hiyo amewaondoa aliekuwa Waziri wa Michezo na Msaidizi wake kufuatia Nchi hiyo kutolewa Hatua ya Makundi ya Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil.Rais John Magama hakutoa sababu zozote ila hatua hii inakuja mara baada ya Ghana kumaliza Nafasi ya mwisho ya Kundi G bila kushinda Mechi yeyote.
Waziri Elvis Afriyie-Ankrah amehashimiwa Wizara nyingine na Msaidizi wake amepelekwa Eneo la Ashanti.Kambi ya Ghana huko Brazil ilikumbwa na migogoro kiasi cha Wachezaji kutishia kugoma hadi Rais Magama alipokodi Ndege kuwapelekea Posho zao ambazo walikuwa hawajalipwa zinazokadiriwa kuwa Pauni Milioni 1.76.
Pia Wachezaji, Sulley Muntari na Kevin-Prince Boateng, walitimuliwa kwenye Kikosi hicho na kusimamishwa kwa muda usiojulikana wakidaiwa kuwa na utovu wa nidhamu.Ilidaiwa Muntari alimpiga Afisa wa Timu hiyo wakati Boateng alimtukana Kocha James Appiah.
Kampeni ya Ghana huko Brazil ilikuwa tofauti kabisa na ile ya Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2010 huko Afrika Kusini walipotolewa Robo Fainali wakiwa nusura ya kutinga Nusu Fainali kama si unyama wa Straika wa Uruguay, Luis Suarez, kuudaka Mpira Mstari wa Goli katika Dakika ya 120.
No comments:
Post a Comment