Kundi D la Fainali za Kombe la Dunia
huko Brazil Usiku Wa Leo zinaanza Mechi zao za kwanza kwa Uruguay kuivaa
Costa Rica huko Estadio Castelão Jijini Fortaleza na kufuatia ule
mtanange unaongojewa kwa hamu, England v Italy.
TAARIFA ZA WACHEZAJI/TATHMINI/REKODI/VIKOSI:
Hali za Wachezaji
Fowadi
wa England Danny Welbeck amepona tatizo lake la enka lakini Alex
Oxlade-Chamberlain bado hajapona maumivu ya Goti lake aliloumia
walipocheza Mechi ya Kirafiki na Ecuador huko Marekani Wiki 2
zilizopita.Italy huenda wakalazimika kutumia
Masentahafu wa 3 nyuma badala ya kusimamisha Difensi ya Mtu 4 baada ya
Fulbeki wao Mattia De Sciglio kuumia Pajani.Lakini habari njema kwa Italy ni zile za Mario Balotelli na Marco Verratti kupata afueni matatizo yao kiafya.
England National Team
Tathmini
Matumaini
ya England ya mafanikio kwenye Mechi za Kimataifa yanaanza na Kikosi
cha Cesare Prandelli, Italy, ambacho ndicho kilichowatoa kwenye
Mashindano ya mwisho makubwa huko kwenye michuano ya EURO 2012
walipobwagwa kwa Mikwaju ya Penati.Kila Timu inatinga ndani ya Arena
Amazônia Jijini Manaus ikihofia athari za Joto na hivyo watacheza Soka
la tahadhari la kumiliki Mpira ili wasiupoteze ovyo na kupoteza nguvu
ovyo kwa kuukimbiza kutaka kuumiliki tena.
Italy National Team
Kama ilivyokuwa kwenye EURO 2012, Mpishi
mkuu wa Italy ni Mkongwe Andrea Pirlo, ambae sasa ana Miaka 35, na
ambae huko Kiev Miaka minne iliyopita alitoa Pasi nyingi kupita Wacheza
wote wa Kiungo wa England na kuzunguka umbali mrefu kupita Mchezaji
yeyote wa England kwenye Mechi hiyo ya EURO 2012.
Mario Balotel
Lakini England ya hivi sasa, chini ya
Meneja Roy Hodgson, ni ya Chipukizi wengi, kina Daniel Sturridge, Raheem
Sterling na Ross Barkley, wakiongezwa nguvu na Wakongwe Steve Gerrard,
Frank Lampard na Wayne Rooney.
Wayne Rooney.
Uso kwa Uso
-Jumla Mechi 24
-England: Ushindi Mechi 8 Magoli: 30
-Sare: 7
-Italy: Ushindi 9 Magoli: 27
Dondoo muhimu
-Mara pekee kwa England na Italy
kukutana kwenye Kombe la Dunia ni kwenye Mechi ya kuwania Mshindi wa
Tatu Mwaka 1990 ambayo Italy walishinda 2-1.
-England wameshinda Mechu 2 tu kati ya 11 walizocheza mwisho dhidi ya Italy wakifungwa 6.
-Mara ya mwisho kukutana ilikuwa huko Switzerland Mwezi Agosti Mwaka 2012 na England kushinda 2-1.
VIKOSI VINAVYOTARAJIWA:
England: Hart, Johnson, Jagielka, Cahill, Baines, Gerrard, Henderson, Lallana, Sterling, Rooney, Sturridge
Italy: Buffon, Abate, De Sciglio, Bonucci, Chiellini, De Rossi, Pirlo, Verratti, Candreva, Marchisio, Balotelli
REFA: Bjorn Kuipers [Holland]
No comments:
Post a Comment