Wakili mmoja nchini Misri amesema kwamba
mahakama imezingatia hukumu ya kifo cha wanachama 182 wa kundi la Muslim
Brotherhood .Washtakiwa hao ni miongoni mwa watu 700
wanaoshtakiwa kwa kukishambulia kituo kimoja cha polisi katika eneo la
Minya mwaka uliopita.
kiongozi wa kundi hilo Mohammed Badie ni miongoni mwa wale waliohukumiwa kifo.Washtakiwa wengine watano walipewa hukumu nyengeine ya kati ya miaka 15 na 55 huku wengine wakiachiliwa huru.Wanachama wa kundi la MUslim Brotherhood wakiwa mahakamani
Hukumu iliotolewa mnamo mwezi Aprili ambapo jaji aliwapatia hukumu ya kifo washtakiwa wote ilizua pingamizi kutoka kwa makundi ya kupigania haki za kibinaadamu.
Source; BBC Swahili
No comments:
Post a Comment