Maelfu ya wanamgambo wa Kishia waliobeba silaha,
wamefanya mhadhara mjini Baghdad na miji mengine ya Iraq ili kuonesha
nguvu zao dhidi ya wapiganaji wa Kisunni ambao wameteka maeneo makubwa
kaskazini mwa Iraq.
Wafuasi hao wa kiongozi wa Kishia mwenye msimamo
mkali, Moqtada al-Sadr, piya walipinga wanajeshi wa Marekani kurudi
Iraq kupambana na wapiganaji.
Kikosi cha Moqtada al-Sad kiliwahi kupigana na Marekani nchini Iraq kwa miaka kadha.Katika mhadhara uliofanywa Kirkuk, mwakilishi wa
Moqtada al-Sad, Raad al Sakhri, alihutubia wafuasi wa jeshi lao
liitwalo Mehdi:
Al-Qaim ni mji muhimu katika kuvuka mpaka ambao unaweza kuwaruhusu wapiganaji wa kundi la ISIS kupitisha silaha nzito, kutoka maeneo ya Syria wanayodhibiti, hadi Iraq.
Kundi hilo piya limesema kuwa limeuteka mji wa Rawa.Na limeeleza kuwa mapambano makali yanaendelea kwenye kinu kikubwa kabisa cha kusafisha mafuta nchini Iraq, Baiji, na wamedungua helikopta mbili za serikali.
Source;BBC Swahili
No comments:
Post a Comment