Herrera, mwenye Miaka 24, amesaini Mkataba wa Miaka Minne kukiwa na Kipengele cha Nyongeza ya Mwaka mmoja zaidi.
Kiungo huyo, ambae sasa anasubiri
Shahada ya Kimataifa ya Uhamisho ilikuubariki kikamilifu Uhamisho huu,
alijiunga na Bilbao Mwaka 2011 akitokea Real Zaragoza na kuichezea Mechi
128 na kufunga Bao 11.
Pia amezichezea Timu za Taifa za Vijana za Spain za chini ya Miaka 20, U-20, na pia U-21 na U-23.Mchezaji huyo anakuwa wa kwanza
kusainiwa chini ya Meneja mpya Louis van Gaal ambae sasa yuko huko
Brazil kama Kocha wa Netherlands.
Akimpokea Mchezaji huyo mpya, Meneja
Msaidizi wa Man United, Ryan Giggs, alisema: “Ander ni Kijana mdogo
hodari mwenye nguvu na ubunifu. Tunaamini yeye ni Chipukizi atakaeng’ara
sana huko Spain na nina hakika atapendwa na Mashabiki wetu. Nimefurahi
ameichagua Manchester United. Nangojea kwa hamu tuwe nae kwenye Ziara ya
kabla Msimu mpya huko Marekani.”
Nae Ander Herrera amesema: “Kusaini
Manchester United ni ndoto iliyotimia. Nimecheza Old Trafford na
Athletic Club kwa Mechi za Ulaya na hiyo ni kumbukumbu kubwa kwangu.
Nimejiunga ili kuisaidia Klabu kutimiza malengo yake yote. Ninafuraha
sasa kuishi Jijini Manchester na nangojea kwa hamu nivae Jezi Nyekundu
inayosifika ya United. Sitasahau muda wangu na Athletic Club na nataka
niwashkuru Mashabiki wote na Wafanyakazi kwa sapoti yao na juu ya yote
nawashkuru Wachezaji wenzangu wa zamani na kuwatakia kila la heri hapo
baadae.”
No comments:
Post a Comment