Sulley Muntari na Kevin-Prince Boateng wamefukuzwa kutoka Kikosi cha Timu ya Ghana kilichopo huko Brazil kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia kutokana na ukosefu wa nidhamu.
Chama cha Soka cha Ghana, GFA, kimethibitisha kufukuzwa kwa Wachezaji hao na kusema pia wamesimamishwa kwa muda usiojulikana.Taarifa hiyo ya GFA ilifafanua kuwa
Boateng alitumia ‘lugha chafu na ya matusi’ kwa Kocha Kwesi Appiah
wakati Muntari alimshambulia na kumpiga Mjumbe wa Kamati Kuu.
Inadaiwa tukio hilo la utovu wa nidhamu lilitokea Jumanne wakati Muntari alipomshambulia na kumpiga Moses Armah.Nae Boateng anadaiwa kutukana Siku hiyo hiyo Mazoezini na hakutaka hata kuomba samahani.
Ghana, ambao Leo hii wanacheza na
Portugal kwenye Mechi ya mwisho ya Kundi ambayo wanatakiwa kushinda huku
Mechi ya Germany na USA iwapendelee, wamekuwa kwenye msukosuko huku
Wachezaji wakidai Malipo yao.
Jana, Serikali ya Ghana ilikodisha Ndege
kwenda Brazil kupeleka Dola Milioni 3 kuwalipa Wachezaji kwani walikuwa
wametishia kugomea kucheza Mechi yao na Portugal.Ili kuingia Raundi ya Pili ya Mtoano
Ghana ni lazima waifunge Portugal na kuombea Mechi ya Germany na USA
itoe Mshindi wa Goli nyingi ili wao wapite kwa ubora wa tofauti ya
Magoli ikiwezekana.
No comments:
Post a Comment