Straika wa zamani wa Brazil Ronaldo
amempongeza Miroslav Klose baada ya Mjerumani huyo kuifikia Rekodi yake
ya Bao 15 za kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
Klose, Miaka 36, alitokea Benchi kwenye
Mechi ya Jana ya Kombe la Dunia huko Brazil na kuisawazishia Germany
walipotoka Sare ya 2-2 na Ghana kwenye Mechi ya Kundi G.
Akiposti kwenye Mtandao wa Twitter, Ronaldo alisema: “Karibu kwenye Klabu. Naifikiria furaha yako. Hili ni Kombe la Dunia bora!”Ronaldo alifunga Goli zake hizo 15 kwenye Fainali za Kombe la Dunia za 1998, 2002 na 2006.
Klose amepia Bao kwenye Fainali za Kombe la Dunia za 2002, Bao 5, zote za Kichwa, Mwaka 2006 Bao 5 na Mwaka 2010 Bao 4.
Vile vile Klose ameifikia Rekodi ya Lejendari wa Brazil Pele na Mjerumani, Uwe Seeler, ya kufunga Bao katikaFainali za Kombe la Dunia 4 mfululizo.
DZEKO AMLAUMU REFA KWA BOSNIA KUTUPWA NJE YA KOMBE LA DUNIA
Bosnia-Hercegovina walitupwa nje ya
Fainali za Kombe la Dunia hapo Jana Jumamosi huko Cuiaba, Brazil baada
kufungwa Bao 1-0 na Nigeria lakini Straika wao, Eden Dzeko, amemlaumu
Refa kwa kushindwa kwao.
Kwenye Mechi hiyo ya Kundi F, Dzeko
alifunga Bao safi Kipindi cha Kwanza lakini Refa Peter O´Leary wa New
Zealand alilikataa Bao hilo kwa madai ni Ofsaidi lakini marudio
yalionyesha Straika huyo wa Manchester City hakuwa Ofsaidi.Nigeria walishinda kwa Bao 1-0 lililofungwa na Peter Odemwingie anaechezea Stoke City huko England.
Bosnia walifungwa Bao 2-1 na Argentina
kwenye Mechi ya Kwanza na hivyo kubakisha Mechi moja ya kukamilisha
Ratiba na Iran huku Nigeria wakicheza na Argentina na kuhitaji Sare au
hata kufungwa ikiwa Iran haitaifunga Bosnia.
Akiongea kwa hasira baada ya Mechi ya
Jana, Dzeko, ambae alidai mbali ya kukataa Bao lao safi hata Bao la
Nigeria lilitokea baada ya Emmanuel Emenike kumchezea Rafu Emir Spahic
kabla hajampasia Mfungaji Odemwingie.
Dzeko alifoka: “Tunarudi nyumbani, tuna
huzuni na Refa pia anastahili kurudi nyumbani kwa sababu alibadilisha
matokeo na ndio maana tumefungwa!”
No comments:
Post a Comment