Kocha mbrazil Marcio Maximo leo amesaini mkataba wa miaka
miwili kwa ajili ya kuwatumikia Mabingwa mara 24 wa Ligi Kuu ya Vodacom timu ya
Young Africans pamoja na msaidizi wake Leonadro Neiva ambao wamesema wamekuja
kuisaidia Yanga iweze kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya
Yanga, Maximo amesema anajiskia furaha sana kurudi kufanya kazi Tanzania, kwani
watu wake ni wakarimu, wapenda mpira hivyo anaona kama yupo nyumbani japo awamu
hii ni kwa majukumu ya ngazi ya klabu tofauti na awali alipokua ngazi ya Taifa.
Nimekuja kufanya kazi na Yanga, nawashukuru viongozi wake
kwa kuamua kuniamini na kunipa nafasi hii, wamenifuatilia kwa awamu tatu
mfululizo na hatimaye safari hii wamefanikiwa kunipata kwa kushirikiana na
wakala wangu Ally Mlei sasa kazi ni moja tu kuijenga Yanga.
"Jumatatu naanza kazi moja kwa moja pamoja na msaidizi
wangu Neiva kwa kushirikiana na kocha wa kikosi cha U-20, wachezaji waliopo na
wachezaji wa kikosi cha U20 watakua wakifanya mazoezi pamoja alisema"
Maximo".
Natambua tuna wachezaji wengi katika timu za Taifa
mbalimbali ikiwemo ya Tanzania (Taifa Stars), Uganda (The Cranes) na
Rwanda (Amavubi) ambao wapo wanayatumikia mataifa yao, na punde watakapomaliza
majukumu hayo wataungana nasi kwa maandalizi.
Kuhusu Kaseja yale yalishapita, najua ni kipa mzuri mwenye
uwezo na uzoefu wa kutosha na kipindi hiki najivunia kuwa na makipa watatu
wenye uwezo mzuri, Yaliyopita Yameshapita yalikuwa ni timu ya Taifa na sasa
tumekutana Yanga kazi yetu ni moja tu kuifanya klabu iwe kwenye hadhi ya
Kimataifa zaidi.
Naye kocha msaidizi Leonado Neiva amesema tumekuja kufanya
kazi, kwa kushirikiana na wachezaji waliopo kutoka sehem mbambali barani Afrika
na Amerika tutapata mchanganyiko mzuri wa uchezaji.
No comments:
Post a Comment