Kombe la dunia Brazil 2014 linatarajiwa kungo'a nanga
baadaye leo jioni huku Brazil na Croatia wakitoana kijasho mjini Sao
Paolo.Dimba hilo litakalodumu kwa mwezi mmoja,
litashuhudia mataifa 32 yakimenyana kuwania kombe hilo katika fainali
itakayochezwa mjini Rio tarehe 13 Julai.
Mwaka jana zaidi ya watu milioni moja walishiriki katika maandamano ya kupinga hatua ya serikali kuandaa michezo hiyo kwa gharama ya juu wakati wananchi wengi wakiishi kwa umasikini.Serikali ya Brazil iko makini kuzuia kutokea tena kwa ghasia zilizoshuhudiwa wakati wa maandamano hayo. Rais Dilma Rousseff amesema kuwa hatakubali kamwe maandamano yanayosababisha ghasia kuathiri kombe la dunia.
Maelfu ya polisi na wanajeshi watashika doria nchini humo kuhakikisha kuwa mechi zinafanyika bila vurufu.
England itacheza mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Italy Jumamosi tarehe 14 .Timu hiyo pia itacheza dhidi ya Uruguay na Costa Rica katika kundi D.
Wenyeji Brazil wataanza mechi leo wakipigiwa upatu kushinda kombe la dunia kwa mara ya sita wakati mabingwa watetezi Hispania nao wanakilenga kushinda kombe hilo kwa mara ya nne baada ya kushinda ubingwa wa Ulaya miaka miwili iliyopita.
No comments:
Post a Comment