Marekani imeituhumu Sudan kwa kufanya mashambulio dhidi ya raia wake katika majimbo ya Kordofan kusini na Blue Nile .Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa ,
Samantha Power amelaani mashambulio hayo ambayo alisema yalilenga shule
na hospitali
Mapema juma hili, mashirika ya misaada yaliliandikia baraza la usalama la umoja wa mataifa, umoja wa Afrika pamoja na jumuiya ya nchi za kiarabu yakitaka mashambulizi dhidi ya raiya yasitishwe na serikali ya Sudan.Bi Power aliilaani kwa matamshi mazito zaidi mashambulizi ya serikali ya Sudan katika eneo hilo.
Bi Samantha Power
Bi Power alilinganisha mbinu za kivita za serikali hiyo na zile zinazotumika katika vita vilivyoharibu sehemu ya Magharibi mwa Darfur, ambapo serikali ililaumiwa kwa kufanya mashambulizi kwa misingi ya kikabila.
“Marekani inatoa wito kwa makundi yote yaliyojihami kusimamisha vita dhidi ya raiya na kutii sharia za kimataifa,” alisema.
No comments:
Post a Comment