Uingereza imesisitiza kuwa marufuku iliyowekewa mmea
wa Miraa itaanza kutekelezwa tarehe 24 mwezi Juni. Hii inafuatia bunge
la nchi hiyo kupitisha uamuzi wa serikali ya Uingereza kuorodhesha miraa
katika kundi la dawa za kulevya.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari Uingereza
imesema kuwa uamuzi huo haulengi Kenya moja kwa moja. Imeongeza kuwa
Serikali ya Uingereza imekuwa ikidhamiria kwa muda mrefu kuchunguza
kisheria hali ya mmea huo.
Mapema mwezi uliopita wabunge kutoka
maeneo ya Meru kunakokuzwa kwa wingi mmea huo walikuwa wametishia
kuwasilisha bungeni hoja ya kuwahamisha waingereza wanaomiliki mashamba
katika maeneo hayo ikiwa Uingereza itapiga marufuku mmea huo.Wabunge hao walikuwa wamesema kuwa wakulima wa
mmea huo watapata hasara kubwa kwa sababu walikuwa wakiutegemea kukuza
uchumi wa eneo hilo.
Miraa ni kitega uchumi kwa wakazi wa eneo la Meru nchini Kenya
Na kwa sababu hiyo Uingereza imesema kuwa
inatambua matatizo yanayowakumbuka wazalishaji lakini itaendelea
kushirikina na serikali ya Kenya kwa kufadhili miradi ya kukuza uchumi.Taarifa hiyo imeongeza kuwa Uingereza ilichukua uamuzi huo baada ya kushauriana na washiriki wake.Nchi nyingi zenye uwezo mkubwa wa kiuchumi yaani
G8 zikiwemo Canada na Marekani zimeharamisha Miraa iliyotajwa kuwa
miongoni mwa dawa za kulevya.
Mswada wa kupiga marufuku mmea huo unaotumia mno
Uingereza ulijadiliwa bungeni machi na kuidhinishwa na bunge la chini
na lile la juu baadaye hivyo kuwa sheria.
No comments:
Post a Comment