Wanamgambo wa kiislam ambao wamedhibiti eneo kubwa la Iraq wanasema sasa wataelekeza mashambulio yao katika mji mkuu Baghdad.Jana kundi lenye uhusiano na mtandao wa
al-Qaeda- ISIS liliteka miji ya Mosul na Tikrit, lakini vikosi vya
serikali vilitumia mashambulizi ya anga kuzuia wanamgambo hao wasisonge
mbele kuelekea katika mji wa Samara
Waziri mkuu wa Iraq, Nouri al-Maliki, anataka bunge kutangaza hali ya tahadhari kusaidia kukabiliana na mzozo huo wa kivita .Lakini mwandishi wa BBC aliye nchini humo
anasema vikosi vya serikali vimeonyesha kutokuwa na uwezo wa kukabiliana
na mashambuliz na hakuna matumaini ya kurejea kwa hali ya utulivu.
Msemaji wa chama cha Dawa cha waziri mkuu wa
Iraq kilichopo na makao London, amesema mzozo huo hautosababisha
kusambaratika kwa serikali ya Nouri Al Maliki.Wananchi wengi wamelazimika kutoroka mji wa Mosul hofu ya kushambuliwa Zuhair Al Nahar amesema itakabiliana na uhasama wa wapiganaji hao.
Wakati huo huo Uturuki imesema kuwa itafanya mashambulio makali iwapo raia wake wanaozuiliwa na waasi wataumizwa.Duru za habari zasema kuwa waasi wameuteka ubalozi wa Uturuki, ulioko Mosul na wanawazuia takriban watu 48.Msemaji katika wizara ya mambo ya nje Marekani, Jen Psaki ameiambia BBC kwamba Marekani ipo tayari kutoa usaidizi.
No comments:
Post a Comment