Rais mpya wa Ukraine ,tajiri Petro Poroshenko ameapishwa rasmi hii leo katika sherehe iliyofanyika katika bunge la taifa hilo mjini Kiev.Katika hotuba yake ya kwanza mda mfupi tu baada ya kuapishwa Poroshenko amesema kuwa anataka kulirudisha taifa hilo katika hali yake ya asili ya Ulaya.
Ameongezea kuwa atatia saini mkataba wa kuwaruhusu raia wa Ukraine kusafiri katika mataifa ya muungano wa ulaya bila vikwazo vyovyote.Amesema kuwa hatua hiyo ndio ya kwanza ya kutaka Ukraine kuwa mwanachama kamili wa muungano wa Ulaya.
No comments:
Post a Comment