Rais Obama amesema anaangalia uwezekano wa kuisaidia
Iraq kukabiliana na mashambulizi ya wanamgambo wa kiislam waonadhibiti
eneo kubwa la kaskazini mwa Iraq .Hata hivyo maafisa wa Marekani wamesema
wanaendelea na majadiliano ili kuona kama wanaweza kutuma vikosi vya
kijeshi katika kukabiliana na kundi hilo.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani Jen Psaki ametoa ufafanuzi akidai kuwa watalaam wao bado wanaendelea na majadiliano na kwamba si nia ya nchi yake kurejesha vikosi vyake Iraq japo kuwa inaona haja ya kutoa msaada kwa nchi hiyo kutokomeza makundi hayo.
No comments:
Post a Comment