Social Icons

Friday, 13 June 2014

Neymar Tegemeo Brazil Aiongoza Vyema mechi ya kwanza ya Ufunguzi,Leo Holland Uso Kwa Uso na Spain


Wenyeji,Brazil, baada ya Sherehe ya Ufunguzi ya Fainali za Kombe la Dunia iliyofana sana,walijikita Uwanjani na kucheza Mechi ya Ufunguzi kwa kuichapa Croatia Bao 3-1.
Croatia ndio waliotangulia kupata Bao kwenye Dakika ya 11 baada ya Krosi ya chini kutoka Winga ya Kushoto kumkuta Fulbeki wa Kushoto wa Brazil Marcelo ambae alitumbukiza Mpira wavuni bila kutegemea.

Neymar-Brazil
-Umri: Miaka 22
-Mechi: 50
-Goli: 33
*AFIKIA REKODI YA MALEJENDARI Ronaldinho & Jairzinho

Supastaa Neymar aliamsha sherehe Uwanja mzima na Nchi nzima ya Brazil baada ya kusawazisha kwenye Dakika ya 29 kwa Shuti la chinichini la Mguu wa Kushoto.Kipindi cha Pili, Brazil walipewa Penati baada ya Beki wa Croatia, Lovren, kumwangusha Fred na Neymar kupiga Bao la Pili.

MAGOLI:
Brazil 3
-Neymar Dakika ya 29 na 71 [Penati]
-Oscar 91
Croatia 1
-Marcelo Dakika ya 11 [Bao la Kujifunga mwenyewe]

Huku Dakika zikiyoyoma na Croatia kujikakamua kutaka kusawazisha, kaunta ataki ya Brazil ilizaa Bao la Tatu kwa kazi njema na ya ufundi ya Oscar.

VIKOSI:
Brazil: Julio Cesar, Dani Alves, Thiago Silva, Luiz, Marcelo, Paulinho, Gustavo, Hulk, Oscar, Neymar, Fred
Akibas: Jefferson, Fernandinho, Dante, Maxwell, Henrique, Ramires, Hernanes, Willian, Bernard, Jo, Maicon, Victor.

Croatia: Pletikosa, Srna, Corluka, Lovren, Vrsaljko, Modric, Rakitic, Perisic, Kovacic, Olic, Jelavic
Akiba: Zelenika, Pranjic, Vukojevic, Schildenfeld, Brozovic, Rebic, Sammir, Vida, Eduardo, Subasic.
Refa: Yuichi Nishimura (Japan)




ROBIN VAN PERSIE ASEMA HOLLAND IKO TAYARI KWA SPAIN

Holland sasa wameerevuka kuikabili Spain kupita Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2010 kwa mujibu wa Nahodha wa Nchi hiyo Robin van Persie.Holland watawavaa Mabingwa Watetezi wa Dunia Spain Leo Ijumaa huko Salvador Nchini Brazil katika Mechi ya Kwanza ya Kundi B ikiwa ni kama marudiano baada ya Nchi hizi kukutana Fainali ya Kombe la Dunia huko Afrika Kusini Mwaka 2010 na Spain kushinda 1-0.

Huko Afrika Kusini, Holland, chini ya Kocha Bert van Marwijk, walifungwa 1-0 katika Dakika za mwisho za Mechi hiyo iliyokwenda Dakika 120 huku Refa Howard Webb wa England akitoa Kadi za Njano 14 na Nyekundu 1 ikiwa ni Rekodi kwa Fainali ya Kombe la Dunia.

Safari hii, Holland wako chini ya Kocha Louis van Gaal na Robin van Persie amesema wao ni Timu nzuri na wana Wachezaji Vijana kupita huko Afrika Kusini na ambao wako tayari kuikabili Spain.Hata hivyo, Van Persie amekiri Spain pia ni Timu nzuri yenye Wachezaji wazuri akiwataja Diego Costa na Mchezaji mwenzake wa Manchester United, Kipa David de Gea.

Uso kwa Uso
-Mechi: 9
-Spain: Ushindi 4
-Netherlands: Ushindi 4
Sare: 1
VIKOSI VINATARAJIWA:
Spain: Casillas, Ramos, Pique, Alba, Martinez, Fabregas, Alonso, Iniesta, Silva,  Costa, Villa
Netherlands: Cillessen; Blind, Indi, de Vrij, Vlaar, Janamat ; de Jong, Sneijder, Guzman ; Robben, Van Persie
REFA: Nicola Rizzoli [Italy]

RATIBA:
JUMAA, JUNI 13, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Mexico v Cameroon
A
Estadio das Dunas
2200
Spain  v Netherlands
B
Arena Fonte Nova
0100
Chile  v Australia
B
Arena Pantanal


JUMAMOSI, JUNI 14, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
REFA
1900
Colombia v Greece
C
Estadio Mineirão
Mark Geiger [USA]
2200
Uruguay v Costa Rica
D
Estadio Castelão
Felix Brych [Germany]
0100
England v Italy
D
Arena Amazonia
Bjorn Kuipers [Holland]
0400
Ivory Coast v Japan
C
Arena Pernambuco
Enrique Osses [Chile]

No comments:

Post a Comment