Kiungo wa Uhispania Xabi Alonso ameafikiana mkataba wa miaka miwili na klabu ya ujerumani Bayern Munich .Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32 amekubali kuondoka Real Madrid katika misimu mwili ijayo.
Xavi
alitokea Liverpool alipojiunga na Real Madrid mwaka wa 2009 na alikuwa
ameongeza muda wa miaka 2 katika mkataba mpya aliotia sahihi mwezi
Januari Bernabeau .Hata hivyo haijabainika ni kwanini anaondoka kutoka kwa mabingwa wa ligi kuu ya Ulaya.
Bayern yaandika mkataba wa miaka 2 na Xavi
Aidha kiungo huyo alikuwa ametangaza kustaafu soka ya kimataifa jumatano baada ya kuichezea Uhispania katika mechi 114.Xavi anatarajiwa kuwahutubia waandishi wa habari ijumaa baada ya kupita uchuinguzi wa siha huko bayern hapo jana(alhamisi).
kiungo huyo ambaye ameshinda kombe la dunia na
Uhispani huko Afrika Kusini mwaka wa 2010 alitokea Real Sociedad kabla
ya kujiunga na Liverpool 2004 alipoisaidia kushinda ubingwa wa bara
ulaya mwaka huo.
No comments:
Post a Comment