Social Icons

Sunday 25 May 2014

Tazama hapa Goli Bora la Muda wote la Mbrazil Bruno Xavier v Germany,Brazil Ilishinda Goli 9-4.


Tumezoea kuona magoli ya ajabu na Bora muda wote lakini hili naweza kusema ni bora zaidi ya yote.Huko Brazil kwenye Beach soccer Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Brazil Bruno Xavier amefunga goli bora la muda wote nakuweka rekodi walipokuwa wakicheza dhidi ya timu ya Taifa ya Ujeruman ambapo Brazil Ilishinda Goli 9-4.

Tazama video ya We Are One (Ole Ola) Pitbul iliyotakiwa kutumika katika kombe la dunia Brazil ft Jenifer Lopez


Tazama hapa video ya wimbo wa Pitbul ft Jenifer Lopez We Are One {Ole Ole} uliotakiwa kutumika katika fainali za kombe la dunia nchini brazil 2014[The Official 2014 FIFA World Cup Song] na badala yake kubadilishwa na kuchukuliwa wa Shakira - La La La

Maoni yawapiga kura yanaonyesha kuwa Poroshenko atashinda kuwa rais Ukraine


Matokeo yanayotokana na maoni ya wapigaji kura yanaonesha kuwa biliyoneya anayetengeneza chakileti, Petro Poroshenko, ameshinda katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais wa Ukraine.

Papa Francis ameombea ukuta wa ukingo wa Magharibi huko Bethlehem


Papa Francis ameombea ukuta wa saruji ambao Israel inajenga kulitenga eneo la ukingo wa Magharibi huko Bethlehem.Aliweka kichwa chake juu ya juu ya ukuta huo, ambapo kumechorwa maneno" ipe uhuru Palestina".

Mbwana Samata ainusuru Tp Mazembe Cuf Champion Ligi


Mbwana Samata Straika mahiri wa Tanzania, Jioni hii huko Stade TP Mazembe, Lubumbashi, Congo DR, alifunga Bao pekee katika Dakika ya 62 wakati Tmu yake TP Mazembe ilipoitungua AS Vita Club, pia ya Congo DR, Bao 1-0 katika Mechi ya KUNDI A la CAF CHAMPIONZ LIGI.

Rapa Wiz Khalifa amedakwa na polisi uwanja wa ndege mjini Texas Baada ya Kukutwa na Bangi


Rapa wa muziki wa nchini Marekani Wiz Khalifa amedakwa na polisi katika uwanja wa ndege mjini Texas baada ya kukutwa na kitu kinachodaiwa kuwa ni bangi wakati wa zoezi la ukaguzi ndani ya mabegi yake.

Baada ya Mechi ya Jana UEFA Kocha wa Spain,Vincente Del Bosque atangaza kikosi cha wachezaji 29 wengine watemwa


Kocha wa Mabingwa wa Dunia Spain,Vincente Del Bosque, amechelewesha kutaja Kkosi chake cha mwisho cha Wachezaji 23 kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil na badala yake amemwita Gerard Deulofeu, aliekuwa Everton kwa Mkopo, na kuwaacha Wachezaji wa Real Madrid na Atletico Madrid kwa ajili ya Mechi ya kujipima nguvu na Bolivia.

Chris Brown - Do Better Feat.Brandy & Lil Wayne,Sikiliza kionjo(Snippet)


Umemisi sauti ya Mkali Wa R&B chris brown akifanya Corabo na Brandy baada ya chris kushirikishwa kwenye Put It Down .very soon Ngoma Itatoka na itaitwa Do Better ft. Brandy & Lil Wayne,kwa sasa sikiliza kionjo cha ngoma hiyo hapa

Yaya Toure Hati Hati Kucheza Fainali za Kombe la Dunia


Shirikisho la Soka la Ivory Coast limethibitisha kuwa Yaya Toure anapatiwa matibabu nchini Qatar kwa majeraha ambayo hayajawekwa wazi kabla ya kujiunga na wachezaji wenzake kwa ajili ya kambi yao ya mazoezi ya Kombe la Dunia iliyopo Marekani. 

HOT BANG!: Akon – Dutch That Sh*t


Ngoma mpya nyingine kutoka kwa Akon inaitwa Dutch that Shit ,unaweza kuisikiliza na kudanload hapa

Baada ya Kutemwa Timu Ya Taifa ya Brazil Ronaldinho Aja kivingine


Baada ya kutemwa katika kikosi cha timu ya ya Brazil na kocha Luiz Felipe Scolari kwa ajili ya Kombe la Dunia, Ronaldinho amekuja na mbinu nyingine ya kumfanya kujipatia kipato katika michuano hiyo ya mwaka huu. 

New Single; Nick Minaj - Pills N Pations Hot Song


Ngoma mpya kutoka kwa Mamber wa YMCMB Nick Minaj - Pills N Pations ,Isikilize na Kuidanload Hapa

Taifa la Ukraine hii leo linashiriki katika shughuli ya uchaguzi wa urais


Taifa la Ukraine hii leo linashiriki katika shughuli ya uchaguzi wa urais uliotajwa kuwa muhimu katika historia ya taifa hilo.Wagombea 18 wanawania wadhfa huo katika raundi ya kwanza ambayo inajiri wakati ambapo vikosi vya serikali vinakabiliana na wanamgambo wanaounga mkono Urusi mashariki mwa taifa hilo.

New Single; Kabaya Ft Cent P - Life Very Hot


Miongoni mwa ngoma kali sana kutoka kwa msanii kabaya aliyomshirikisha Cent P ni hii inaitwa LIFE, chukua time yako kuisikiliza na kudanload Hapa ni Joint Ya ukweli sana .cheki hapa

Mahakama kuu nchini Malawi yamuhukumu Rais Joyce Banda


Mahakama kuu nchini Malawi imetoa hukumu dhidi ya jaribio la rais Joyce Banda kupiga marufuku matokeo ya shughuli ya uchaguzi wa urais na ubunge.Mahakama imeiagiza tume ya uchaguzi nchini humo kuendelea na shughuli ya kuhesabu kura.

Tazama Come Back ya Real Madrid Dhidi ya Atletical UEFA,Diego Simeone Akiri Kujisikia Uchungu Baada Ya Kipigo


Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone amekiri kuwa anasikia uchungu baada Jana Usiku Mahasimu wao wakubwa Real Madrid kutwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI walipotoka nyuma kwa Bao 1-0 na kushinda 4-1 kwenye Fainali iliyochezwa Mjini Lisbon, Ureno na kwenda hadi Dakika 120 baada ya Sare ya 1-1 katika Dakika 90.

Saturday 24 May 2014

David Luiz Aaga Chelsea Kuelekea Paris Saint-Germain


David Luiz hii Leo alikuwa Jijini Paris akikamilisha taratibu zake za kuhamia Paris Saint-Germain na akiwa huko alitoa salaam za shukrani kwa Klabu yake Chelsea ambako kuna taarifa Mmiliki wa Klabu hiyo Roman Abramovich ametoa idhini kuwa Dau la kumuuza Mbrazil huyo apewe Jose Mourinho kununua Wachezaji wapya.

Rais Joyce Banda wa Malawi aamuru kusitishwa kwa shughuli ya kuhesabu kura


Rais Joyce Banda wa Malawi ameamuru kusitishwa mara moja kwa shughuli ya kuhesabu kura na kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo ulifanyika jumanne iliyopita.

Bobby Zamora Airejesha QPR Ligi kuu England Apiga Goli Dakika 90 Tazama Hapa


Bao la dakika ya 90 la Bobby Zamora limewarudisha Queens Park Rangers LIGI KUU ENGLAND Msimu ujao baada ya kuifunga Derby County Bao 1-0 kwenye Fainali ya Mechi za Mchujo za Daraja la Championship

Mbeya City Yaanza Vyema Huko Khartoum, Sudan


Huko Khartoum, Sudan zimesema Wawakilishi wa Tanzania Bara kwenye Michuano ya CECAFA NILE BASIN, Mbeya City, Leo hii wameanza vyema Masindano hayo kwa kuichapa Academie Tchite ya Burundi Bao 3-2 kwenye Mechi ya KUNDI B.Kwenye Mechi hii, Bao za Mbeya City zilifungwa na Paul Nonga, Mwegane Yeya na Themi Felix.

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ameapishwa kwa muhula wa pili


Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ameapishwa kwa muhula wa pili wa uongozi.Maelfu ya wafuasi, wakipepea bendera za taifa, walishangilia ndege za jeshi za Afrika Kusini zilipopita juu ya uwanja wa sherehe.

Habari Kuhusu Al Shabaab Kushambulia bunge la Somalia


Kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Al Shabaab limeshambulia bunge la Somalia na kusababisha vifo vya watu kadhaa mjini Mogadishu.Milipuko na milio ya risasi imesikika huku bunge likishambuliwa, wabunge wakiwa ndani kwa mkutano.

Friday 23 May 2014

ICC Yamuhukumu miaka 12 jela Kiongozi wa zamani wa wapiganaji waasi DRC Germain Katanga


Mahakama ya kimataifa ya jinai ICC imemhukumu kiongozi wa zamanai wa wanamgambo waasi katika Jamuhuri ya kidemokrasi ya Kongo, Germain Katanga, kifungo cha miaka kumi na miwili jela baada ya kumpata na hatia ya uhalifu wa kivita.

Tazama Hapa Video ya Show Ya Diamond Akiwa London


Diamond alikwenda London Uingereza kushoot video ya kolabo yake mpya na Iyanya lakini pia akafanya show kwa wabongo na fans wake wengine kwenye mji huohuo.Ni moja kati ya show kali mno

Umoja wa mataifa walaani Sera Za Kanisa Katoliki


Umoja wa mataifa umetuhumu makao makuu ya kanisa katoliki la Vatican kwa kuidhinisha na kutumia sera zilizowezesha mapadre kubaka na kuwalawiti maelfu ya watoto.Kamati ya umoja wa mataifa ya haki za watoto imesema kanisa hilo linapaswa kuondoa wote wanaokiuka haki za watoto kutoka nafasi za uongozi na kuanzisha uchunguzi dhidi yao.

Tetesi za Usajili Louis Van Gaal Amkataa Toni Kross,David Luiz Kutimkia PSG


Toni Kross hatajiunga na Manchester United Msimu huu baada ya Louis Van Gaal kumkataa lakini PSG wako mbioni kumsaini Beki wa Chelsea David Luiz kwa Pauni Milioni 50 na Bacary Sagna anategemewa kuhamia Manchester City.Hizi ndio habari zinazovuma huko England.

Thursday 22 May 2014

Tazama Hapa Video ya Wimbo Wa Kombe la Dunia jina la La La La (Dare) Mastaa kadhaa waonekana


Ule wimbo maalum kwa ajili ya michuano ya kombe la dunia mwaka 2010 wa ‘wakawaka’ ulioimbwa na Shakira ambapo this time kwenye kombe la dunia baada ya ule kufanya vizuri… mwaka huu Shakira amepata shavu jingine la kufanya wimbo wa kombe la dunia litakalofanyika Brazil kuanzia mwezi ujao.

Tuesday 20 May 2014

Luis Enrique Meneja mpya Barcelona kwa Mkataba wa Miaka wa miwili


Barcelona jana imemteua Luis Enrique kama Meneja wao mpya kwa Mkataba wa Miaka wa miwili.Luis Enrique, Miaka 44, anambadili Gerardo Martino ambae Juzi alitangaza kuachia ngazi baada ya kushindwa kuisaidia Barca kutetea Taji lao la La Liga.

Kuhusu Oscar Pistorius Kufanyiwa Uchunguzi wa akili


Jaji katika kesi inayomkabili Oscar Pistorius anasema kuwa mwanariadha huyo lazima aanza kufanyiwa uchunguzi wa kiakili kuanzia Jumatatu wiki ijayo kwa mwezi mmoja kubaini hali ya akili yake alipomuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.

Monday 19 May 2014

Wanawake waonyesha hisia za kimapenzi na mapadre wa kikatoliki waandikia barua kwa Papa Francis


Kundi moja la wanawake walio na hisia za kimapenzi na mapadre wa kikatoliki wamemuandikia barua kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ya kumtaka kubadilisha sheria za kanisa hilo zinazowazuia viongozi hao wa dini kuoa.

Klabu moja huko Bolivia (Sport Boys) imemsajili rais wa Bolivia Evo Morales Tazama Mshahara wake


Klabu moja huko Bolivia (Sport Boys) imemsajili rais wa Bolivia Evo Morales kucheza kama kiungo cha kati kuanzia Agosti mwaka huu.Rais Morales atalipwa mshahara wa dola $213 kwa mwezi .Morales atavalia jezi nambari 10 katika klabu hiyo iliyoko Kusini mwa Bolivia katika jimbo la Santa Cruz.

Official Louis van Gaal Meneja mpya Manchester United


Manchester United imethibitisha kuwa Louis van Gaal ndie Meneja wao mpya na Ryan Giggs atakuwa Msaidizi wake.Van Gaal amepewa Mkataba wa Miaka Mitatu na ataanza rasmi kazi yake Old Trafford baada ya Netherlands kumaliza kampeni yao kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil ambako yeye ndie Kocha wao Mkuu.

Sunday 18 May 2014

Sababu zilizo Mfanya Gerardo Martino Kuachia Ngazi Barcelona


Gerardo Martino ataacha kazi ya Ukocha wa Barcelona mara baada ya Jana kupokonywa Ubingwa wa La Liga baada kutoka Sare 1-1 na Atletico Madrid ambao wameutwaa Ubingwa huo na kuiacha Barca ikitoka mikono mitupu Masimu huu kitu ambacho hakijawahi kutokea tangu 2007/08.

Mabingwa wa Italy Juventus Wafunga Msimu Kwa Rekodi


Huko Turin, Italy, Mabingwa Juventus wameweka Rekodi katika Ligi Kubwa Ulaya kwa kumaliza Msimu na na kuzoa Pinti 102 baada ya kuichapa Cagliari Bao 3-0.Ingawa walikuwa tayari wameshatwaa Ubingwa, Juventus, chini ya Meneja Antonio Conte, waliingia kwenye Mechi hii na Cagliari wakiwa na ari kubwa ya ushindi na mapema tu Frikiki ya Andrea Pirlo ilimbabatiza Kipa Marco Silvestri na kutinga.

Taifa Stars Yafanya Kweli Uwanja Wa Taifa


Tanzania, ikicheza Nyumbani Jijini Dar es Salaam, Leo imeifunga Zimbabwe Bao 1-0 katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Pili ya Mtoano ya AFCON 2015 kuwania kucheza Fainali huko Morocco Mwaka 2015.

New Single; Kabaya,G.Solo,X.O Ft Addy- Wikiend



Ningoma kali ambayo imefanywa na upcoming Artist kutoka njombe icheki hapa ni bonge la track Mimi nimewaelewa Najua ipo siku watasikika .

Nchi za Balkan Zakumbwa na Mafuriko Makubwa


Juhudi za kuyadhibiti mafuriko mabaya zaidi ambayo yamewaathiri maelfu ya raia wa mataifa ya Balkan zinaendelea.Mto wa Sava tayari umevunja kingo zake katika miji mingi na sasa ni tishio kwa kiwanda kikubwa cha umeme nchini Serbia.

Taarifa kuhusu Raia wa China Kujeruhiwa Vietnum


Shirika rasmi la habari nchini Uchina Xhinua limesema kuwa serikali imewaondoa zaidi ya raia wake 3000 kutoka nchini Vietnam kufuatia ghasia dhidi raia wa Uchina nchini humo.

New Video Kid Ink feat. Chris Brown & Tyga - Main Chick REMIX


Moja kati ya wanamziki wanao fanya vizuri hivi sasa Marekani na duniani kwote ni KID INK hasa kupitia ngoma yake aliyompa shavu Chris Brown .Show me. sasa Tazama video yake mpya hapa ya wimbo wake ambao ni RMX  Main Chick feat. Chris Brown & Tyga ..Tazama hapa

Saturday 17 May 2014

Atletical,Arsenal na Beyern zafurahia Wikiend kwa Vikombe .Tazama magoli jinsi yalivyopatikana hapa


Atletical madrid Leo wametwaa Taji la Ubingwa wa Spain kwa mara ya kwanza baada ya Miaka 18 baada ya kutoka Sare ya Bao 1-1 na Barcelona waliokuwa wakicheza kwao Uwanjani Nou Camp.

Tazama Hapa video mpya ya Ommy Dimpoz – Ndagushima


Kituo pekee cha TV kilichourusha huu wimbo kwa mara ya kwanza ni MTV BASE May 16 2014 ambapo unaweza kuitazama video hii  Addy-Tz baada ya kuachiwa rasmi May 17 2014.Itazame hapa

La Liga Bingwa Kupatikana Leo Nou Camp FC Barcelona v Atletico de Madrid


Leo, kuanzia Saa 1 Usiku,FC Barcelona wanaingia Uwanjani kwao Nou Camp kucheza na Atletico Madrid wakijua ushindi kwenye Mechi hii ya mwisho ya La Liga utawapa Ubingwa wao wa 5 huko Spain katika Miaka 6.

Rais Obama amkaribisha Waziri Mkuu Mteule wa India Narendra Modi Mjini Washington


Kuna mwamko mpya wa kisiasa nchini India ambapo chama cha kitaifa cha Hindu ,BJP kimeshinda uchaguzi uliokuwa na maamuzi makali kuwahi kufanyika nchini humo kwa kipindi cha miongo mitatu.Chama cha Congress ambacho kimelitawala taifa hilo kwa kipindi kirefu cha miaka 67 tangia uhuru wa taifa hilo kilishindwa vibaya.

Ripoti kutoka Kenya Watu kumi Wauwawa kwa Milipuko Miwili,Marekani Yawaondoa Wananchi wake Kenya


Milipuko miwili ilitikis Soko kubwa la nguo la Gikomba mjini Nairobi na kuwaua watu 10 huku zaidi ya hamsini wakijeruhiwa.Soko hilo linapakana na mtaa wa Easleigh ambako wasomali wengi  wanaishi na kufanya kazi.Shirika la serikali la kushughulikia majanga linasema kuwa angalau watu 10 wamefariki na wengine zaidi ya hamsini kujeruhiwa.

Romelu Lukaku kutolewa Sadaka kwa Atletico Madrid


Klabu ya Chelsea imemtoa sadaka Romelu Lukaku kwa Atletico Madrid ikiwa ni sehemu ya juhudi zao za kutaka kumsajili Diego Costa. Costa ni mchezaji anayepewqa kipaumbele na kocha Jose Mourinho katika uasajili wa kiangazi na anataka biashara hiyo ikamilike haraka.

Friday 16 May 2014

Manchester City Yaadhibiwa na UEFA kwa kukiuka Sheria Ya FFP


Manchester imepewa Adhabu na UEFA kwa kukiuka Sheria za FFP [Financial Fair Play] ambazo zinataka Klabu zijiendeshe kwa Mapato yao wenyewe kwa kupigwa Faini ya Pauni Milioni 49 na Kikosi chao kubanwa kisizidi Wachezaji 21 na 8 kati yao ni lazima wawe Wachezaji Chipukizi waliokuzwa Nyumbani kwenye Mechi zao za UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao.

Vichwa vya Habari vya Magazeti Ya Leo 17 May 2014


Kama hujapata time ya kupitia vichwa vya habari vilivyogonga magazeti ya leo pitia hapa sasa magazeti yote ikiwemo Sakata la ugombea uongozi simba,Bifu zito Etoo na Morinho,Habari kuhusu milipuko miwili iliyotokea kenya jana na Kauli ya mama Maria Nyerere

NEW SONG AUDIO: DUSSE - LIL WYNE



Jumamosi kesho Wembley Stadium Jijini London Fainali ya FA CUP Arsenal vs Hull City tazama Tathimini Hapa


Watu wengi huko Uingereza hii ni nafasi murua kwa Arsene Wenger na Arsenal yake kumaliza ukame wao wa Miaka 9 bila ya Kombe lolote wakati Jumamosi watakapoingia Wembley Stadium Jijini London kuivaa Hull City kwenye Fainali ya FA CUP.

Tazama hapa vikosi vya timu za Taifa 32 zitazoshiriki kombe la Dunia Nchini Blazil zinazoanza 12 Juni 2014

  
Nchi zote 32 ambazo zipo kwenye Fainali ya Kombe la Dunia huko Brazil zinazoanza Juni 12 zimetangaza Vikosi vyao vya Awali visivyozidi Wachezaji 30 ambavyo ifikapo Juni 2 kila Timu inapaswa kuwasilisha FIFA Listi ya Wachezaji 23 tu.Baadhi ya Nchi, moja kwa moja, zimetangaza Wachezaji 23 lakini nyingine zimetaja na Wachezaji wa Listi ya Akiba.

Chama cha upinzani nchini India BJP kimeshinda uchaguzi mkuu


Chama cha upinzani nchini India BJP kimeshinda uchaguzi mkuu kwa kupata idadi kubwa zaidi ya kura kuliko chama kingine chochote.Kiongozi wa chama BJP Narendra Modi,amesema kuwa wananchi wajiandae kwa mambo mazMatokeo ya awali yalionyesha kuwa chama hicho kimepata kura nyingi kiasi cha kuweza kutawala bila ushirikiano wowote na chama kingine.