Social Icons

Thursday 11 December 2014

Diamond kashinda Channel O, Idris BBA, huyu mwingine kaipa Tanzania headlines hizi nzuri saa kadhaa zilizopita.


Jana December 10 2014 Watanzania walimpokea kwa shangwe mwakilishi wao kwenye BBAHotshots Afrika Kusini, Idris ambae ndie alitangazwa mshindi wa dola za kimarekani laki tatu siku kadhaa tu baada ya Diamond kuing’arisha Tanzania kwa kushinda tuzo 3 za Channel O.

Tazama jinsi Nyota wa NBA LeBron James avunja kanuni za kifalme


Mchezaji wa mpira wa vikapu LeBron James alivunja protokali au kuvunja kanuni za maadili ya kifalme alipomshika mabegani Kate Middleton akiwa na majasho kwenye jezi lake huku mumewe Kate, Prince William akifanya mzaha kuhusu ukubwa wa mguu wa mchezaji huyo huku wote wakiangua kicheko.

Monday 6 October 2014

Arsene Wenger Diego Costa ni mshambuliaji hatari


Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa Diego Costa ni mshambuliaji hatari
na kwamba mshambuliaji huyo wa Chelsea ni tishio

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta Aachia Madaraka Tayari Kutua ICC

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema yuko radhi kwenda katika mahakama ya kimataifa ya ICC kwa kikao maalum kuhusu kesi inayomkabili.

Sunday 5 October 2014

Sirea A | Juventus Yaendeleza Ubabe Yainyuka 3-2 AS Roma ..Tazama hapa Matokeo Mechi Zote


Mabingwa wa Italy Juventus, wakicheza kwao Juventus Stadium Jijini Turin, Usiku huu wamewabwaga AS Roma ambao walikuwa wamefungana nao kileleni mwa Ligi Serie A Bao 3-2 na kupaa zaidi kileleni.

VPL | Yanga yapanda Hadi nafasi ya 3 Ligi kuu England,Yanyakua point 3 Kutoka kwa Jkt Ruvu


Hii Leo, huko Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Yanga wameichapa JKT Ruvu Bao 2-1 na kukwea hadi Nafasi ya 3 ya Ligi Kuu Vodacom Yanga walifunga Bao lao la kwanza Dakika ya 32 kupitia Kelvin Yondani na Bao hilo kudumu hadi Haftaimu.

Vita ya Wenger v Morinho Yamalizika kwa Arsenal Kupigwa Goli 2-1 Yashuka hadi nafasi ya 6,Waziri Mkuu Costa Afanya Kweli


Chelsea wameendelea kujichimbia kileleni mwa Ligi Kuu England walipoichapa Arsenal Bao 2-0 huko Stamford Bridge hii Leo.

David Degea Shujaa Manchester United Akamata Penalt Wachopa hadi nafasi ya 4,Di Maria na Falcao Wapeleka Kilio Everton


Manchester United wakicheza Uwanjani kwao Old Trafford wameifunga Everton Ba0 2-1 katika Mechi ya Ligi Kuu England huku Kipa wao David De Gea akiwa Shujaa kwa kuokoa Penati na Bao kadhaa lakini aliewapa ushindi ni Straika Radamel Falcao

Story Kuhusu Kijana Aliyeamua Kumuoa Mama Yake Wa Kambo Ipo Hapa


Bwana mmoja nchini Ufaransa amemuoa mke wa zamani wa baba yake (mama yake wa kambo) baada ya kushinda kesi iliyodumu kwa miezi kadhaa.

NEW MUSIC | Rick Ross - Keep Doin That (Rich Bitch) (feat. R. Kelly).mp3 Sikiliza na Danload hapa


Rick Ross ameachia ngoma yake aliyompa shavu R.Kelly inayoenda kwa jina la  Keep Doin ThatUtakao patikana kwenye  forthcoming Hood Billionaire Albam yake. 

Cheick Tiote na Tuhuma za Ndoa ya Mitara Tazama hapa alichokisema

Hivi karibu gazeti la The Sun liliripoti juu ya tuhuma za kumhusu kiungo wa timu ya Newcastle Cheick Tiote na familia yake.

Ngome Ya Mwisho ya Al-Shabaab yadhibitiwa na Vikosi vya Serikali Pamoja na Wanajeshi wa Muungano Wa Africa

Mji wa bandari wa Barawe nchini Somalia ambao ulikuwa umetajwa kuwa ngome ya mwisho ya kundi la Al shabaab umethibitiwa na vikosi vya serikali vikisaidiwa na wanajeshi wa muungano wa Afrika.

Saturday 4 October 2014

Arsenal, Galatasaray, FC Basel Na Borussia Dortmund Kuadhibiwa na UEFA

Klabu za Arsenal na Galatasaray zitakabiliwa na adhabu kutoka kwenye shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, kufuatia fujo za mashabiki zilizojitokeza wakati wa mchezo wa kundi la nne uliozikutanisha klabu hizo usiku wa kuamkia jana jijini London.

Picha | Birthday Party Ya Diamond Platnumz,Alipewa zawadi ya gari jipya aina ya BMW X6 Tazama Hapa

Diamond Platinumz jana usiku alisherehekea siku yake ya kuzaliwa akitimiza umri wa miaka 25.Sherehe hiyo ilifana ambapo mama yake mzani na mpenzi wake Wema Sepetu pamoja na ndugu, jamaa na marafiki waliohudhuria waliinogesha sherehe hiyo iliyomalizika majira ya saa kumi alfajiri.

P Diddy J Lo anamfunika Kim Kardashian kwa 'makalio', J Lo nae amzungumzia P Diddy

Rapper mkongwe mwenye mafanikio makubwa, P Diddy juzi alimwagia sifa aliyekuwa mpenzi wake enzi hizo Jennifer Lopez akieleza kuwa alikuwa mwenye bahati sana kuwa nae.

Kivumbi EPL Manchester United wanataka kulipa kisasi kwa kufungwa na Everton ni Kesho Jumapili Uwanjani Old Trafford


Hii ni Mechi ambayo Manchester United wanataka kulipa kisasi kwa kufungwa na Everton Mechi zote mbili za Ligi Kuu England Msimu uliopita kitu ambacho huko nyuma kilikuwa adimu kutokea.

EPL | Dabi ya London Jumapili CHELSEA vs ARSENAL Tazama Tathimini na Hali za Vikosi Hapa


HII ni Dabi ya Jiji la London na hii ni moja ya Mechi kubwa za Msimu wa 2014/15 wa Ligi Kuu England wakati Stamford Bridge itakapo waka moto Jumapili kwa Mechi kati ya Chelsea na Arsenal.

BUNDERSLIGA | Borussia Dortmund wameendelea kuwa nyanya Ligi Kuu Ujerumani Msimu huu

Borussia Dortmund wameendelea kuwa nyanya kwenye Bundesliga Msimu huu baada kuchapwa 1-0 wakiwa Uwanjani kwao Signal Iduna Park na SV Hamburg.Hii ni Mechi ya 4 sasa ya Ligi ambayo Dortmund hawajaonja ushindi na Bao la Leo lililowamaliza lilifungwa na Pierre-Michel Lasogga katika Dakika ya 35.

LA LIGA | Mabingwa Watetezi Atletico Madrid wapigwa Bao 3 na Vinara wa Ligi, FC Barcelona, washinda Bao 2


LA LIGA Leo hii ilishuhudia Mabingwa Watetezi Atletico Madrid wakipigwa Bao 3-1 na Vinara wa Ligi, FC Barcelona, wakishinda Bao 2-0.Atletico, wakicheza Ugenini, walichapwa na Valencia Bao 3-1 na Wenyeji hao kupata Bao zao zote 3 ndani ya Dakika 13 za kwanza kwa Bao za Joao Miranda, aliejifunga mwenyewe Dakika ya 6, Andre Gomes Dakika ya 7 na lile la Dakika ya 13 la Nicolas Otamendi.

Louis van Gaal Juan Mata atambadili Nahodha Wayne Rooney Old Trafford Jumapili ,Nahodha Hajulikani


Louis van Gaal amedokeza Juan Mata atambadili Nahodha Wayne Rooney wakati Manchester United inacheza na Everton Uwanjani Old Trafford kwenye Mechi ya Ligi Kuu England lakini alikataa kusema nani atakuwa Kepteni wa Mechi hiyo.

EPL | Liverpool, Hull, Sunderland Ushindi Leo,Yaya,Aguero Waipa City Ushindi | Ratiba Ya Kesho Hapa


EPL,Bao za Mohamed Diame na Nikica Jelavic zimewapa ushindi Hull City walipocheza kwao na Crystal Palace naoMABINGWA Watetezi Manchester City wameshinda Bao 2-0 kwa Bao za Dakika za mwishoni walipocheza na Aston Villa huko Villa Park

Ligi Kuu Vodacom | Costal Pekee Yashangilia Ushindi Wengine Sare ,Simba Yajikongoja Droo 3 Mfululizo | Ratiba ya Kesho Hapa



Ligi kuu VODACOM imeendelea Leo hii na Mechi pekee iliyotoa mshindi ni ile ya kule Mkwakwani Jijini Tanga Coastal Union ilipoifunga Ndanda FC Bao 2-1.

Stephen Keshi kuendelea kuinoa Timu Ya Taifa Ya Nigeria


Stephen Keshi amesema kuwa ataendelea kukisimamia kikosi cha soka nchini Nigeria katika mechi ya kuwania taji la ubingwa barani Afrika dhidi ya Sudan licha ya kuwa hajasaini kandarasi mpya.

Muingereza mwengine akatwa kichwa na Kundi la Wanamgambo wa Islamic state

Kundi la wanamgambo wa kiislamu la Islamic state limetoa ukanda wa video unaoonyesha mateka Alan Henning raia wa Uingereza akikatwa kichwa.

Kuhusu Mwanamke mmoja Sweden kujifungua mtoto kutokana na kizazi alichowekewa kupitia upasuaji


Mwanamke mmoja nchini Sweden amejifungua mtoto kutokana na kizazi alichowekewa kupitia upasuaji.Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 36 alizaliwa bila kizazi kabla ya kuwekewa kizazi cha mwanamke aliyekuwa katika miaka yake ya sitini.

Friday 3 October 2014

Muendelezo wa ligi Mbalimbali barani ulaya Tazama hapa ratiba za Ligi Hiyo



Muendelezo wa ligi Mbalimbali unaendelea wikiendi hii katika viwanja vya ligi mbalimbali barani ulaya Tazama hapa ratiba za Ligi Hiyo

Viongozi Wa China Wasema Maandamano Ya Hong Kong Yataambulia Patupu

Viongozi wa Uchina wanasema kuwa maandamano ya kupigania haki ya kuimarisha demokrasia katika eneo la Hong Kong yataambulia patupu.Taariri yenye matamshi makali katika Gazeti la Kikomunisti ilikariri kuwa Serikali inaendelea kumuunga mkono Mkuu wa eneo la Hong Kong, CY Leung.

Hamisi Tambwe Guda Guda Kuivaa Stand United na Si Majeruhi Kama Ilivyoarifiwa Awali


Mshambuliaji wa kutumainiwa wa Timu ya Simba Hamisi Tambwe leo hasubuhi amefanya mazoezi kwa asilimia 100 na kuondoa uvumi uliokua umemuhusisha kukosa mechi ya kesho dhidi ya stand united

Messi matatani kwa kukwepa kodi Apelekwa Kizimbani ,,,Tazama Hapa

Nyota wa timu ya Barcelona na Argentina Lionel Messi anakabiliwa na mashtaka ya ukwepaji wa kodi,hii ni kwa mujibu wa jaji mmoja wa Uhispania.

Tazama Hapa Picha za programu mpya ya Windows 10 ambayo imeipiku Windows 9 Iliyozinduliwa na Kampuni ya Microsoft


Kampuni ya Microsoft imezindua programu mpya ya Windows 10 ambayo imeipiku Windows 9.Kampuni hiyo pia inatarajia wateja wake watarudi kwani wengi walikuwa wakisitasita kuboresha oparesheni zao tangu Windows 8.

Ndoa Yavunjika Kutokana na Tofauti za Kidini Nchini India..Story Kamili Ipo Hapa


Maafisa wa polisi katikati mwa India wamefutilia mbali harusi kati ya mwanamume mkristo na mwanamke wa kihindu baada ya shinikizo kutoka kwa makundi ya kihindu yenye mrengo wa kulia.

DUNIANI | Tazama Picha ya Kiti Kinacho Punguza Upweke Hapa


Kuna wakati kila mmoja maishani pengine huhitaji kupata 'hug' (kukumbatiwa) ili kujisikia sio mpweke. Sasa kampuni moja nchini Japan imetengeneza kiti maalum ambacho kitakuwa tayari wakati wowote kumkumbatia na kumliwaza mtumiaji.

Thursday 2 October 2014

Maajabu ya Dunia | Tazama hapa Sokwe wabunifu Waanzisha Tabia Mpya Mwituni


Watafiti wamegundua kifaa kipya kinachotumiwa na idadi kubwa ya Sokwe ,Wanasema kuwa kifaa hicho ni ishara tosha kwamba Sokwe wa mwituni wameanzisha tabia mpya.

Kiongozi Wa Boko Haram Atoa Tamko na Akana Kufa Asema 'Sijafa' | Story Yote Hapa



Kanda ya video inayomuonyesha mtu anayedaiwa kuwa kiongozi wa kundi la Boko Haram imetolewa akikana madai ya jeshi kwamba amefariki.Katika kanda hiyo,Abubakr Shekau anasema kuwa wapiganaji wake waliitungua ndege ya wanajeshi wa angani iliotoweka wiki tatu zilizopita.

UEFA | Wenger: Welbeck ana kasi ya umeme | Tazama hapa Video ya jinsi alivyofunga magoli 3 Kama hukuona


Mkufunzi wa kilabu ya Arsenal nchini Uingereza Arsene Wenger amemtaja mshambuliaji wake Danny Welbeck kama mchezaji mwenye kasi ya 'umeme' baada ya kuifungia timu ya Arsenal mabao matatu siku ya jumatano katika mechi ya kilabu bingwa barani Ulaya dhidi ya Galatasaray.

Saturday 30 August 2014

New Music | Kipaji Cha Ajabu Katika Muziki Bongo | G the Gunner | For Ma People


Muziki umekuwa na ushindani mkubwa sana hivi sasa na kila kukicha vipaji huzaliwa tumeona marekani kunavipaji vilivyofanya vizuri sana katika musiki mfano Kendrick Lamar na wengine Wengi Hapa Bongo Pia kunawatu kama Young Killer na Wengine Wengi

Tazama Hapa Ratiba Ligi kuu England ( EPL ) Wikiendi Hii


Burudani ya Mechi za Wikiendi ni kuwashuhudia Washambuliaji watatu 3 Walio Sajiliwa kwa Kishindo katika ligi hiyo ...Angel Di Maria- Manchester United, Mario Balotelli- Liverpool na Samuel Etoo- Everton...Je??? Etoo kuwachachafya Chelsea ....Wakati Huo huo Straika wa Chelsea Diego Costa huenda Atakuwa nje ya Uwanja kwa Muda wa Wiki Nne 4.

Torres amua kuondoka Chelsea – Atua Rasmi Ac Millan

Fernando Torres amemaliza kipindi kigumu kabisa cha miaka mitatu na nusu kwenye maisha yake ndani ya klabu ya Chelsea baada ya kukubali kuondoka katika timu hiyo.

Ivory Coast kususia mechi Dhidi ya Sierra Lion AFCON


Shirikisho la soka la Ivory Coast limesema kuwa huenda likasusia mechi ya kufuzu kwa dimba la mabingwa barani Afrika dhidi ya wapinzani wao Sierra Leone ikihofia kuenea kwa Ebola.

Bayern yamsajili Kiungo Wa Real Madrid Xavi Alonso


Kiungo wa Uhispania Xabi Alonso ameafikiana mkataba wa miaka miwili na klabu ya ujerumani Bayern Munich .Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32 amekubali kuondoka Real Madrid katika misimu mwili ijayo. 

Sunday 29 June 2014

Ripoti kutoka Iraq zinaarifu kuwa vikosi vya serikali vyashindwa kuteka Tiqrit Vyarudi Nyuma


Ripoti kutoka Iraq zinaarifu kuwa vikosi vya serikali vilivyojaribu kuuteka mji wa Tikrit kutoka kwa wapiganaji wa kisunni vimelazimika kurejea nyuma.

Taarifa Kuhusu Zaidi ya Watu 130 wahofiwa kufukiwa na kifusi cha jengo lililoporomoka nchini India


Maafisa nchini India wamesema wanahofu kuwa zaidi ya watu 130 wamenasa kwenye kifusi cha jengo lililoporomoka kusini mwa India,takriban Watu watano wameripotiwa kupoteza maisha katika tukio hilo mjini Porur.

Van Gaal Ahitaji Kopo La Maji Uwanjani Raundi ya Pili Katika Mchezo Dhidi Ya Mexico

Kocha wa Uholanzi Louis van Gaal anatarajia shirikisho la soka duniani FIFA litawaruhusu wachezaji wake kunywa maji katika mechi yao ya raundi ya pili dhidi ya Mexico itakayochezwa katika uwanja wa Castelao ulioko katika eneo la Fortaleza.

Beyonce na Jay Z Watoa Mshtuko Mwingine kwa Mashabiki Wao Kwenye Ziara Yao Ya Muziki Ya On The Run Inayoendelea , Tazama Hapa


Ikiwa wamewashangaza mashabiki wao kwa kuonyesha video ya harusi yao iliyofungwa mwaka 2008 na kuzaliwa kwa mtoto wao Blue Ivy, sasa Beyonce na Jay Z wametoa mshtuko mwingine kwa mashabiki wao kwenye ziara yao ya muziki ya On The Run inayoendelea.

Saturday 28 June 2014

Kombe La Dunia Penalti Zaiokoa Brazil , Rodriguez Awaadhibu Uruguay Colombia Robo Fainali Kucheza na Brazil


Kocha wa Brazil Luiz Felipe Scolari amesema Timu yake imebakisha Gemu 3 kufika ’Peponi’ baada Jana kuibwaga Chile kwa Mikwaju ya Penati 3-2 baada ya Sare ya Bao 1-1 katika Dakika 120 za Mchezo za Mechi ya Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia.

[EXCLUSIVE] NEW VIDEO | BEN POL FT JOH MAKINI-UNANICHORA | OFFICIAL VIDEO



NEW MUSIC | Meek Mill | Lay Up (Remix) Feat. Rick Ross | Jay-Z | Trey Songz Very Hot Danload



NEW MUSIC | Lil Wayne | Krazy ..Isikilize na Danload Hapa | Hot Music


Rapper Lil Wayne Ameachia Ngoma Mpya Kama Muendelezo wa Kuiandaa Albam Yake Mpya Inayoitwa Carter V na Ngoma Hii Inaitwa  Krazy na Miongoni mwa Track Zitakazo Husika katika Albam Hiyo .

Ripoti Kutoka Ghana | Rais Awaondoa Aliekuwa Waziri wa Michezo na Msaidizi Wake Baada Ya Kuondolewa Kombe la Dunia


Ripoti toka Ghana zimedai kuwa Rais wa Nchi hiyo amewaondoa aliekuwa Waziri wa Michezo na Msaidizi wake kufuatia Nchi hiyo kutolewa Hatua ya Makundi ya Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil.Rais John Magama hakutoa sababu zozote ila hatua hii inakuja mara baada ya Ghana kumaliza Nafasi ya mwisho ya Kundi G bila kushinda Mechi yeyote.

Taarifa Kuhusu Mwanamume mmoja Aliyelazwa Hospitali Baada Ya Kumkana Mungu


Mwanamume mmoja katika jimbo la Kano, nchini Nigeria, amepelekwa katika kituo cha matibabu ya kiakili baada ya kusema kuwa hamwamini Mungu.Taarifa hii ni kwa mujibu wa shirika moja lisilo la kiserikali nchini nIGERIA.