Madrid return: Real president Florentino
Perez has hinted they could bid for Monaco and Colombia striker Radamel
Falcao next summer
RAIS wa Real Madrid, Florentino Perez
amesema kwamba mapato ya klabu yake tajiri zaidi duniani yanaweza
kumnunua mshambuliaji wa Monaco, raia Colombia, Radamel Falcao mwakani.
Akizungumza katika chati ya shoo ya
soka, Punto Pelota jana usiku, Perez alitolea nje uwezekano wa usajili
wa Falcao katika dirisha dogo Januari, lakini akasema Real lazima iwe
karibu naye mwishoni mwa msimu.
Falcao, mwenye umri wa miaka 27,
aliondoka kwa wapinzani wa Jiji wa Real, Atletico kwenda kujiunga na
Monaco mwishoni mwa msimu uliopita kwa dau lililoripotiwa kuwa kiasi cha
Pauni Milioni 53.
Tuko njiani: Falcao akipiga penalti
alipoichezea Colombia mechi ya kufuzu Kombe la Dunia na Chile mjini
Barranquilla Ijumaa timu hizo zikitoka sare ya 3-3.
"Yeye (Falcao) hatakuja Januari, lakini
Juni, nani anafahamu?"alihoji Perez. "Hakuna kisichowezekana na kuna
muda wa kutosha kutoka sasa hadi huko.
"Falcao ni mchezaji mkubwa na ninajua anataka kucheza (Real) Madrid. Ninatambua hilo, lakini ni kawaida. Wameniambia,".
Mipango kamambe: Rais wa Real,
Florentino Perez akiwa mchezaji ghali duniani aliyesajiliwa kwa Pauni
Milioni 86, Gareth Bale. Sasa anataka Falcao awe Galactico mpya
Yuko juu: Mchezaji mwenye thamani ya
Pauni Milioni 53, Falcao tayari ameifungia mabao saba katika klabu yake
mpya, Monaco msimu huu
Sababu moja kubwa Real kuingia sokoni kusaka mshambuliaji ni kushuka kwa kiwango cha mshambuliaji wake Mfaransa, Karim Benzema.
Kipenzi hicho cha Perez, Benzema
ameshindwa kuteka hisia za mashabiki wa Real tangu awasili mwaka 2009 na
hana furaha sana mbele ya umati wa Bernabeu.
Perez amekuwa akimtetea mshambuliaji
huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye amekuwa akilaumiwa na kocha wa
Real, Carlo Ancelotti kwa kutojituma kiasi cha kutosha uwanjani.
Hali tete: Mshambuliaji Karim Benzema
amekuwa akikandiwa na mashabiki Uwanja wa Bernabeu na kocha wake, Carlo
Ancelotti chini anamlaumu kwa kutojituma kiasi cha kustosha uwanjani
No comments:
Post a Comment