Social Icons

Tuesday 29 October 2013

Chris Brown matatani kwa mara nyingine kwa kumpiga ngumi mtu mmoja huko Washington

chrisJapokuwa bado yupo kwenye probation lakini Chris Brown bado anaendelea kuvunja sheria za huko Marekani. Sources mbalimbali kutoka kwenye mitandao ya uhakika huko zinasema kwamba Chris amekamatwa pamoja na bodygurd wake baada ya Chris mwenyewe kumpiga ngumi ya uso na kumvunja pua jamaa mmoja waliyekutana kwenye hotel.

Picha za ajali ya pili aliyoipata David Beckham na mwanae


7
Staa wa soka David Beckham (38) pamoja na mtoto wake wa kwanza aitwae Brooklyn walipata ajali ndogo nje ya nyumba yao huko Beverly Hills Marekani baada ya gari lao kugongana na gari jingine wakati wakitoka nyumbani.
Hakuna alieumia kwenye hii ajali ambayo iliihusisha Range Rover ya Beckham yenye thamani ya dola za Kimarekani elfu 75 ambapo iliumia sehemu ya mbele na mashuhuda wanasema baada tu ya ajali David Beckham hakuondoka kwenye eneo la tukio, alichofanya ni kusubiri Polisi.

Sunday 20 October 2013

PICHA YA LEO !!!!! Kelly Rowland icheki hapa...

Ufoo Saro Afunguka!!!!!!!!!!!!!!!

Ufoo Saro: “Nyumbani kwetu, pale Kibamba si mbali sana na barabarani, wakati nikikaribia kufika barabarani wakati huo nikitokwa na damu nyingi huku nikihisi tumbo langu limejaa sana nilikutana na dada mmoja ambaye nilimuomba khanga ili nijifunge kuzuia damu zisitoke kwa wingi”.

Anasema dada yule alimpa khanga akajifunga na aliposogea barabarani alikutana na gari lililokuwa likiendeshwa na mwanamke mmoja.

“Nilipoona kuna gari linapita nikainuka kuomba msaada. Liliposimama nilimuona mwanamke akiendesha nikamweleza kwamba nilikuwa nimepigwa risasi na nilikuwa nikiomba msaada wake anikimbize hadi katika hospitali ya Tumbi na kwamba akifika pale tu aniache mlangoni.

“Si rahisi kuamini, yule mama alikataa kunisaidia akisema alikuwa akiwahi sehemu kumchukua mzazi. Sina la kusema niliamua kumsamehe tu yule mama ingawa niliumia sana,”!

Endelea kusoma => http://bit.ly/179MYXz
Ufoo Saro: “Nyumbani kwetu, pale Kibamba si mbali sana na barabarani, wakati nikikaribia kufika barabarani wakati huo nikitokwa na damu nyingi huku nikihisi tumbo langu limejaa sana nilikutana na dada mmoja ambaye nilimuomba khanga ili nijifunge kuzuia damu zisitoke kwa wingi”.

Alicho kiandika ZITTO KABWE kupitia ukurasa wake wa facebook, Fuatilia hapa.....


Flamini kitendawili Ligi ya Mabingwa.

Kocha wa Arsenal,Arsene Wenger amesisitiza kuwa kiungo wake,Mathieu Flamini yupo kwenye hatihati kubwa ya kukosa mchezo wa Ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Borussia Dortmund wiki ijayo.

Roma yaendeleza ushindi Seria A.

Klabu ya Roma imeendeleza wimbi lake la ushindi kwa mechi ya nane mfululizo mara baada ya kuifunga Napoli goli 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Ya Italia”Seria A” Ijumaa Usiku.

Barca yavutwa shati,Atletico Madrid kipigo cha kwanza.

Klabu ya Barcelona ilipata sare yake ya kwanza msimu huu ilipokuwa ugenini ikicheza dhidi ya Osasuna huku Atletico Madrid ikipokea kichapo cha kwanza kutoka kwa Espanyol katika Ligi Kuu ya Uhispania.

Cheki msimamo wa ligii kuu vodacom Tanzania bara na Jinsi Shabiki wa Yanga akiwa amebebwa kwenda kupewa huduma ya kwanza mara baada ya kuzimia wakati timu yake ilipokuwa ikiongoza kwa goli.




#   Team MP W D L GoalsGD Pts
1 Azam FC 10 5 5 0 159 20
2 Mbeya City 10 5 5 0 136 20
3 Simba SC 9 5 4 0 2012 19
4 Yanga SC 9 4 4 1 187 16
5 Mtibwa S 10 4 4 2 154 16
6 Kagera S 9 4 2 3 103 14
7 R.Shooting 10 3 4 3 112 13
8 JKTRuvu 10 4 0 6 9-2 12
9 Coastal U 9 2 5 2 71 11
10 Ashanti Utd 10 2 3 5 9-9 9
11 Rhino 9 1 5 3 8-3 8
12 Prisons 9 1 4 4 5-7 7
13 JKT Oljoro 10 1 3 6 8-8 6
14 Mgambo 10 1 2 7 3-15 5

Rapper D Knob Kutoka Tanzania Amefungua Mtandao Wa Biashara


 


Beyonce Akining'inia Kwenye Moja Ya Majengo Marefu New Zealand


Beyonce alivyokuwa kwenye ziara yake kwenye kisiwa cha New Zealand alipata nafasi ya kwenda kwenye moja ya majengo marefu kisiwani  humo yanayo toa huduma ya kupoteza Uwoga wa Anga. Beyonce alifungwa kamba sehemu muhimu kwenye mwili wake zitakazo weza kumshika wakata anashuka kwa kamba kwenye jengo hilo. Beyonce alivyokamilisha safari hii anasema kwa sasa hana hofu ya anga tena

BEST FM B TWENTY 20 AUGUST 2013






Future achukua hatua za kufungua mashataka akitaka kulipwa fidia dola 1.5 million baada ya kutolewa kwenye tour ya Drake.

future-drake
Future msanii ambaye ni boyfriend wa Ciara, zilitoka taarifa kwamba ametoswa kwenye tour ya Drake iliyopewa jina la “Would You Like a Tour”. Kabla ya kutolewa ilitangazwa kwamba atakuwepo kwenye hiyo tour.

BEST FM B TWENTY 13 AUGUST 2013






Matokeo ya Simba vs Yanga Oct 20 2013,



6Ni mechi ambayo inaingia kwenye kumbukumbu za Watanzania wanaozifatilia hizi timu mbili sana ambapo mpaka kipindi cha kwanza kinaisha Yanga ilikua inaongoza kwa kuwa na magoli matatu huku Simba ikiwa haina hata moja ila kwenye kipindi cha pili Simba wakarudisha magoli yote aisee.
Magoli ya Yanga yamefungwa na Ngassa kwenye dakika ya 15 na mengine mawili yamefungwa na Kiiza dakika ya 35 na 45 ambapo magoli ya Simba yamefungwa na Mwombeki dakika ya 54, Owino 57 na Kaze 83.

Saturday 19 October 2013

HEMEDY PHD AWAOMBA LADHI FANS WAKE KWA KUTOONEKA MR BLUE KWENYE VIDEO YA WIMBO WA REST OF MY LIFE.

 
The Hit Maker wa Track ya Rest Of My Life nazingine Kibao ''Hemedy PHD'' Aliyomshirikisha Mr Blue Amewaomba Ladhi Mashabiki wake kwa Kutooneka Mr Blue kwenye Video ya Wimbo Huo ambayo imeachiwa Rasmi Leo.

Hemedy amesema kuwa Kutokana na Mr Blue Kuwa na Tour nyingi nje ya Nchi ndiyo sababu kubwa iliyofanya Mr Blue kutoonekana kwenye Video hiyo hii nikutokana na yeye Kutaka kuwahi kuitoa Video Hiyo.

PHD Ameongeza Kuwa Licha ya Video hiyo kutoka lakini atafanya Version ya Pili ambayo itamuhusisha Mr Blue na inatarajiwa kuanza kufanyika mapema kabla ya Mwaka Huu Kuisha itakuwa Tayari imetoka.

Akipiga Stori katika Kipindi Cha BEST REQUEST kinachorushwa na BEST FM ya Mkoani Njombe wilaya ya Ludewa amesema anampango wa Kurelease New Joint nyingine ambayo amemshirikisha Bi - Dadakuwa na Mapema Mwazoni mwa Mwaka 2014 ataachia Filamu yake ambayo kwasasa Inafanyiwa uhariri/Editing.

Alicho-post Wema Sepetu kwenye Instagram kinachomhusu Diamond


wema11Wema Sepetu mwenyewe anajua kwamba watu wengi wanafikiri yeye anawaza kuwa na Diamond hivi sasa,

Friday 18 October 2013

NDEGE YA FASTJET YASHINDWA KUTUA MWANZA BAADA YA UMEME KUZIMIKA


KUZIMIKA kwa taa katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza juzi kulisababisha ndege ya fastjet kushindwa kutua na kulazimika kurejea jijini Dar es Salaam.

Inaelezwa kwamba ndege hiyo iliyopaswa kutua saa 2 usiku kwenye uwanja huo ikitokea jijini Dar es Salaam, ilishindwa

 kutua na kulazimika kuzunguka hewani mara tano, hali inayodaiwa kuleta taharuki miongoni mwa abiria.

Habari zinadai kuwa kukosekana kwa umeme katika uwanja huo kulisababisha kutokuwapo kwa mawasiliano, hivyo kuzua tafrani kubwa kwa baadhi ya abiria.

Icheki hapa habari inayogusa zaidi tanzania leo


 

Dk Magufuli aibuka upya 

Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal akikagua ujenzi wa nyumba 851 kwa ajili ya kuuzia wafanyakazi wa serikali baada a kuweka jiwe la msingi jana  katika eneo la Mabwe Pande Jijini la Dar es Salaam. . Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli. Picha na Salim Shao

'Miili ya magaidi yapatikana Westgate'



Wanajeshi wa Kenya wakati waliopokuwa wakizingira Kituo cha Biashara cha Westgate kilichoshambuliwa na magaidi

Miili miwili iliyoungua vibaya aliyoopolewa katika eneo la kituo cha biashara cha Westgate nchini Kenya siku ya Alhamisi inawezekana kwa kiasi kikubwa ikiwa ni ya magaidi walioshambulia kituo hicho, Mbunge mmoja wa Kenya ameiambia BBC.
Ndung'u Gethenji mwenyekiti wa kamati ya Bunge inayochunguza shambulio hilo pia amesema mwili mwingine ambao umepatikana unawezekana kwa kiasi kikubwa ukawa ni wa mmoja wa wanajeshi.

Askari wa Angola waripotiwa kuingia Kongo Brazaville

Afisa wa ngazi za juu wa Kongo Brazaville amesema kuwa, wanajeshi wa Angola wamevuka mpaka na kuingia katika ardhi za nchi hiyo jirani mapema wiki hii na kukamata kikundi cha askari wa Kongo. Kanali Christian Sansa kamanda wa jeshi la Kongo Brazaville amesema kuwa, wanajeshi wa Angola waliingia katika wilaya ya Kimongo kutokea Cabinda na kudai kwamba walikuwa katika ardhi yao.

Iraq yanunua silaha za mabilioni ya dola kwa Russia

Russia imeanza kusafirisha silaha kuelekea Iraq chini ya makubaliano ya kihistoria ya ununuzi wa silaha za mabilioni ya dola yaliyofikiwa kati ya pande mbili mwaka uliopita. Ali al Musawi mshauri wa masuala ya habari wa Waziri Mkuu wa Iraq Nour al Maliki amesema,

Misri yaafiki Ethiopia kujenga bwawa Mto Nile


Afisa mmoja wa Misri amesema kuwa serikali ya mpito ya nchi hiyo imeafiki uamuzi wa Ethiopia kujenga bwawa katika Mto Nile. Gazeti la al Sha'ab al Jadid huku likimnukuu afisa huyo limeandika kuwa, baada ya kukubali mabadiliko yaliyofanywa na Ethiopia kuhusu ujenzi wa bwawa la an Nahdha katika Mto Nile,

MAN UNITED, CHELSEA WALIE TU, LEWANDOWSKI AMEKWISHAMALIZANA NA BAYERN NA ATAPEWA PAUNI MILIONI 10 KUSAINI TU

 Anahama: Robert Lewandowski amefikia makubaliano ya kupewa karibu Pauni Milioni 10 za dau la usajili na Bayern
MSHAMBULIAJI Robert Lewandowski atapokea dau la usajili la karibu Pauni Milioni 10 atakapojiunga na Bayern Munich kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu.
Mabosi wa Allianz Arena wamepuuzia madai kwamba mshambuliaji huyo wa Borussia Dortmund ana fikra mbadala juu ya kujiunga na Bayern na wamesistiza watamalizana naye wakati wa mwaka mpya.

Mchezaji WA Newcastle United apewa ‘Deal’ ya kuigiza Movie ya X!

the-magpies-have-enjoyed-many-exciting-european-nights-including-famous-clashes-with-barcelona-one-of-which-featured-a-certain-tino-asprilla-1354337

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Newcastle United Faustino Asprilla amepwa ofa ya kuigiza filamu za ngono na kampuni moja inayojihusisha na utengenezaji wa filamu hizo nchini Colombia .

Thursday 17 October 2013

Ndoa Ya Producer Timbaland Hatarini

 Mke wa mtayarishaji muziki Timberland, Monique ameripotiwa kuanzisha mchakato wa kuachana na producer huyu na hii ikiwa ni baada ya miaka 5 ya kuishi pamoja kama mke na mume.

Rapper Octopizzo Kwenye Collabo Na Msanii Mkubwa Wa Nigeria.

Octopizzo rapa anayefanya poa sana katika gemu Afrika Mashariki anazidi kuongeza idadi za kolabo na wasanii mbalimbali barani Africa na habari iliyopo ni kwamba rapa huyo amepiga kolabo na mwanamuziki mkongwe wa nchini Nigeria, King Sunny Ade.

Rapper Wa Muda Mrefu Snoop Dogg Amebadilisha Jina Mara Nyingine Tena, kuanza kujiita SnoopZilla

Rapper Snoop Dogg Aka Calvin Cordozar Broadus Jr amebadilisha tena jina lake na kuanza kujiita SnoopZilla.  Rapper huyu mwenye miaka 41 amebadilisha jina hilo ili kutangaza zaidi project yake mpya anayofanya na mwimbaji Dam-Funk, na itaitwa 7 Days of Funk.

cheki Picha, Video Ya Future Anayo Shiriki Star Miley Cyrus

 
Boy Friend wa Ciara, Future yupo mbioni kumaliza video yake mpya inayoitwa Real & True ambayo mpaka sasa imeanza kushika vichwa vya habari baada ya picha za video model wa video hio ambaye ni Miley Cyrus.  

Picha zilizo vuja zinaonyesha msanii Miley Cyrus amepakwa rangi ya silver kwenye mwili wake wote. Fahamu kuwa hapo Miley Cyrus yupo uchi kabisa kama alivyo zaliwa na ndio mwongozaji wa video hio alitaka iwe hivyo.

Video: Sugua gaga (Teaser) - Shaa


kama hukuskia basi ndo unajua sasa kuwa Shaa kwa sasa amesign mkataba wa miezi 6 kuwa chini ya uongozi wa mtu mkubwa fella (mkubwa na wanawe)
na sasa tunaanza kuona matunda ya uongozi huo.... hii ni teaser tu ya ujio mpya wa Shaa, wimbo unaitwa "sugua gaga" ...kaa tayari kwa ujio wake mpya chini ya mkubwa na wanawe.

Picha, Red Carpet Ya BET HipHop Music Awards 2013.


2 Chainz Kwenye Tuzo za BET Hiphop Music Awards jana, Picha Za Wasanii Wengine, Bonyeza Read More.

Wednesday 16 October 2013

Tuesday 15 October 2013

Izzo bizness akutana na Mzee Zahir Zorro Studio....Fishcrab tusubiri NEW JOINT

Studio....Fishcrab....Mchana wa leo Na Mzee Zahir Zorro...Najisikia Furara kufanya kazi na LEGEND...#bless

Hiki ndicho alicho kiandika Lady Jaydee kupitia ukurasa wake wa facebook

MUNGU yupo na humsaidia kila mtu kwa muda na nafasi yake. Usiharakishe mambo, pengine kuna mazuri zaidi kakutengea. :)Relax

FERGUSON AMPA ONYO MOYES.

 
MENEJA wa zamani wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson ametuma ujumbe wa onyo kwa mrithi wake David Moyes kuwa siri kubwa ya mafanikio Old Traford ni umoja na maelewano haswa katika vipindi vigumu. 

MESSI AANZA MAZOEZI.


MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi amempa ahueni kocha wake Gerardo Martino jana wakati aliporejea mazoezini mazoezini baada ya kupota majeraha ya msuli yaliyokuwa yakimsumbua.

RAIS REAL MADRID ATANGAZA AZMA YA KUMSAJILI FALCAO AUNGANE NA RONALDO, BALE


Madrid return: Real president Florentino Perez has hinted they could bid for Monaco and Colombia striker Radamel Falcao next summer
  Madrid return: Real president Florentino Perez has hinted they could bid for Monaco and Colombia striker Radamel Falcao next summer
RAIS wa Real Madrid, Florentino Perez amesema kwamba mapato ya klabu yake tajiri zaidi duniani yanaweza kumnunua mshambuliaji wa Monaco, raia Colombia, Radamel Falcao mwakani.
Akizungumza katika chati ya shoo ya soka, Punto Pelota jana usiku, Perez alitolea nje uwezekano wa usajili wa Falcao katika dirisha dogo Januari, lakini akasema Real lazima iwe karibu naye mwishoni mwa msimu.
Falcao, mwenye umri wa miaka 27, aliondoka kwa wapinzani wa Jiji wa Real, Atletico kwenda kujiunga na Monaco mwishoni mwa msimu uliopita kwa dau lililoripotiwa kuwa kiasi cha Pauni Milioni 53.

LEWANDOWSKI AIKANA BAYERN MUNICH, SASA ATAKA KUCHEZA ENGLAND...NA MAN UTD, MAN CITY ZOTE ZAMTAKA, PATAMU HAPO!

MSHAMBULIAJI Robert Lewandowski amezipa nafasi klabu za Manchester United, Manchester City na Chelsea za England kugombea saini yake, baada ya kusema ameghairi kwenda Bayern Munich.
Mpachika mabao huyo wa Poland, ambaye anatarajiwa kucheza dhidi ya England Uwanja wa Wembley leo, alifikiriwa atajiunga na mabingwa hao wa Ulaya kama mchezaji huru msimu ujao.
Lakini nyota huyo wa Borussia Dortmund amekanusha kufikia makubaliano ya kusaini Mkataba na Bayern na amesema angependa kuchezea klabu moja kubwa ya England.

Rapper Kala Jeremiah sasa ni balozi wa Pepsi, asaini mkataba mnono haujawahi kutokea kwake



Leo hii Rapper Kala Jeremiah amesaini mkataba na kampuni SBC kupitia kinywaji chake cha Pepsi na kutangazwa rasmi kuwa balozi wa Pepsi nchini, na yuko tayari kwa ajili ya kuanza kufanya kazi za kibalozi kuanzia time hii.
 namshukuru sana mungu, lakini nawashukuru sana mashabiki wangu, kwasababu bila wao nisingeweza kuchaguliwa kuwa balozi, wale watu huwa wanaangali unakubalikaje kwenye jamii lakini unajiheshimu vipi katika jamii, nashukuru pia vyombo vya habari kwa kunipigania mpaka kujulikana kwenye makampuni makubwa kama hayo.
Kala alikataa kuzungumzia mtonyo alioupata kutokana na mkaba huo na kusema kuwa hawezi kutaja na itabaki kuwa siri yake, ila hajawahi kusaini mkataba mnono kama huu ni kwa mara ya kwanza kusani mkataba mnono kama huo.

Rihanna azuru South Africa Baadhi ya picha zake akiwa South Africa!

According to MTV BASE ni kwamba Mrembo RiRi kwenye show aliyoifanya juzi Johannesburg, inaaminika kwamba ameweka rekodi kwa kuwa msanii wa kike kupata watu wengi kwenye uwanja wa FNB Jumapili ya 13 October ambapo idadi aliyoipata ni ya zaidi ya watu elfu tisini (90)

October 16 2013 RiRi atafanya show huko Capetown South Africa ambapo wakati akiwa bado S.A  ameendelea kutokelezea kwenye picha kadhaa kama hizi akiwa na Wanyama  mbalimbali.

Rapper Kutoka West Coast The Game ni Cashmoney sasa hivi

Ni shangwe tu ndani ya  Cashmoney … baada ya watu kama Busta kujiunga na CashMoney, na sasa  kwenye headlines ni The Game kujiunga rasmi na Cashmoney baada ya mchongo  huu kutajwa sana kwa zaidi ya miezi 11 ikiwa chini kwa chini

Sunday 13 October 2013

Happy Nyerere day, angalia documentary ya maisha ya mwalimu Nyerere – “The legacy of Julius Nyerere”

Tukiwa tunakumbuka na kusherekea maisha ya Baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere, unaweza kuangalia hii documentary inayohusu maisha ya mwalimu kuanzia alipozaliwa hadi alipoanza harakati za siasa. Siku kama ya leo natumaini  haya yatakuwa material mazuri kwa ajili yako, enjoy.

Baada ya CASSIDY na MEEK MILL sasa ni Diss Nyingine Ya 50 Cent Kutoka Kwa Rapper Game.

Diss nyingine kutoka kwa rapper Game kwa 50 Cent na this time inahusu kurudi G Unit. Rapper Game amelianzisha tena na hasimu mwenzake 50 Cent kwa kumtaja yeye na kundi lake la G Unit kwenye wimbo wa 'Hollywood' Ambao upo kwenye mixtape yake mpya ya "OKE". Joint hii Imetoka October 11 na kashirikishwa rapper Scarface.
Kwenye wimbo Game anasema “Hub City thugs wit me, buck 50,” “Reunite with G-Unit, bitch fuck 50”

Ishu nzima kuhusu mwandishi wa ITV Ufoo Saro kujeruhiwa kwa risasi

Mwandishi wa ITV Ufoo Saro amejeruhiwa kwa risasi iliyopigwa na mwanaume mmoja alieripotiwa kutokua na maelewano mazuri ambapo kwenye hili tukio mwanaume huyu alimpiga risasi na kumuua mama mzazi wa Ufoo Saro.

Mwanaume huyu alimpiga Ufoo risasi mbili ambazo zilimjeruhi na kudhani kwamba amemuua na kisha yeye mwenyewe kujipiga risasi na kufariki.

Saturday 12 October 2013

YANGA YAUA KAGERA, SHUJAA NGASSA NA KIIZA, SIMBA SC YAENDELEA KUNG'ARA KILELENI

YANGA SC imeshinda mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ugenini msimu huu baada ya kuilaza Kagera Sugar mabao 2-1 Uwanja wa Kaitaba, Bukoba jioni hii, wakati watani wao wa jadi, Simba SC pia wameshinda 1-0 dhidi ya Prisons Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Uwanja wa Taifa, bao pekee la Simba SC limefungwa na Jonas Mkude dakika ya 62, wakati Uwanja wa Kaitaba, mabao ya Yanga yamefungwa na Mrisho Ngassa dakika ya kwanza na Hamisi Kiiza 57, wakati la Kagera limefungwa na Godfrey Wambura dakika ya 47. Coasal Union na Ashanti zimetoka 1-1 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. HABARI ZAIDI ITAFUATIA.

ENGLAND YAIFUMUA MONTENEGRO 4-1 NA SASA WABISHA HODI BRAZIL 2014

ENGLAND imeongeza matumaini ya kufuzu Kombe la Dunia baada ya kuifumua Montenegro mabao 4-1 usiku huu.
Mabao ya England inayofundishwa na Roy Hodgson yamefungwa na Rooney dakika ya 48, Boskovic akajifunga dakika ya 62, Townsend dakika ya 78 na Sturridge dakika ya 90 kwa penalti, lakini la wageni limefungwa na Damjanovic dakika ya 71.

VAN PERSIE AVUNJA REKODI YA MABAO YA KLUIVERT UHOLANZI AKIFUNGA HAT TRICK USIKU HUU

Kiwango cha dunia: Robin van Persie sasa ni mfungaji bora wa kihistoria Uholanzi
MSHAMBULIAJI Robin van Persie amekuwa mfungaji bora wa kihistoria wa Uholanzi kufutaia kufunga mabao matatu peke yake (hat trick) usiku huu katika ushindi wa 8-1 dhidi ya Hungary.
Mshambuliaji huyo wa Manchester United aliingia katika mchezo huo wa kufuzu Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil, akiwa ana mabao 38 katika mechi 78 za Orange, na wenyeji hawakuwa na presha kwa kuwa walikwishajihakikishia tiketi ya Brazil Septemba mwakani.

Taarifa kuhusu Henry Joseph wa Simba


Imefahamika kwamba kiungo mkongwe wa Simba Henry Joseph ataendelea kubaki kwenye timu B na huo ni uamuzi wa benchi la ufundi la timu hiyo.
Kocha Msaidizi wa Simba Jamhuri Kihwelo anasema Henry atabaki hapo hadi atakapobadilika ‘anatakiwa kubadilika na kuonyesha juhudi kwamba alikuwa anacheza nje basi atuonyeshe kweli anastahili kuwa katika timu ya kwanza na atatoa msaada’
“Hatujapenda vyombo vya habari kuandika vitu tofauti kama vile kufukuzwa Simba na vinginevyo, tulichofanya ni kwa manufaa ya Simba, kama Henry angekua anajituma wala kusingekuwa na tatizo, tunajua alikuwa Ulaya na ndio maana tunategemea mchango mkubwa kutoka kwake’ – Julio.

Thursday 10 October 2013

NEW,,Joint: Monifere - Gosby feat Vanessa Mdee na Jux

Gosby amedondosha mzigo mpya "Monifere" akiwa na Vanessa Mdee pamoja na Jux, kazi ikiwa imefanyika Bhits chini ya producer Harmy B. 

Lulu ajichora tatto baada ya watu kumhukum na kutamka kumuachia Mungu jukumu hilo



Msanii wa Bongo Movie Tanzania, Elizabeth Michael "Lulu" ameamua kuchora tattoo iliyoandikwa "Only God Can Judge Me" chini ya
shingo upande wa bega lake la kushoto, baada ua kuona watu wamekuwa wakimhukum kwa mambo ayafanyao kulliko Mungu ambae ndie mwenye cheo chake, na kuwataka watu kumuachia jukumu hilo Mungu pekee, na kucha kujipa u-busy usio wa lazima ,

Baada ya kukutana na picha yake hotelini hiki ndicho alichokifanya Diamond katika hoteli aliyofikia

Diamond Platnamz ambae yuko Hongkon kwa sasa, ameamua kutia saini kwenye moja ya picha yake aliyokuta imebandikwa katika ukuta wa hoteli moja ya ki-africa, kuonyesha shukrani kwa mmiliki wa hoteli hiyo.  Kwambaaali kama naiona picha ya Wema Sepetu, sasa sijui na yeye amesaini, lol, tutajua baadae