Mpachika mabao huyo wa Poland, ambaye
anatarajiwa kucheza dhidi ya England Uwanja wa Wembley leo, alifikiriwa
atajiunga na mabingwa hao wa Ulaya kama mchezaji huru msimu ujao.
Lakini nyota huyo wa Borussia Dortmund
amekanusha kufikia makubaliano ya kusaini Mkataba na Bayern na amesema
angependa kuchezea klabu moja kubwa ya England.
Atahamia Ligi Kuu England? Mshambuliaji
wa Borussia Dortmund, Robert Lewandowski (kushoto) amekanusha kuwa na
mpango wa kuhamia Bayern Munich
Mshambuliaji wa nguvu: Lewandowski (kulia), akipambana na Edmar Holovsky wa Ukraine
"Nitakuwa tayari kusaini Mkataba (na
klabu yoyote) ifikapo Januari, lakini sijawahi kusema kwamba nitasaini
mkataba na Bayern," alisema Lewandowski, mwenye umri wa miaka 25.
"Yalikuwa ni maelewano mabaya. Ni kweli
nilipata nafasi ya kuzungumza Sir Alex Ferguson (mwaka jana), lakini
hatukuzungumzia usajili. "Siku moja ningependa kucheza Ligi Kuu England. Nitakuwa na uzoefu mkubwa.'
Mkataba wa Lewandowski katika klabu
yake, Dortmund unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu na klabu zote
za Manchester na Chelsea zimekuwa zikimmezea mate mkali huyo wa mabao
kwa muda sasa.
Mkali wa mabao: Lewandowski (kushoto)
amekuwa mmoja wa washambuliaji tishio Ulaya baada ya kuisaidia Borussia
Dortmund kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita
Leo Wembley tena: Lewandowski aliondoka
na maumivu mara ya mwisho alipocheza Uwanja wa Wembley baada ya
Borussia Dortmund kufungwa na Bayern Munich katika Fainali ya Ligi ya
Mabignwa
No comments:
Post a Comment