EPL,Bao za Mohamed Diame na Nikica Jelavic zimewapa ushindi Hull City walipocheza kwao na Crystal Palace naoMABINGWA Watetezi Manchester City wameshinda Bao 2-0 kwa Bao za Dakika za mwishoni walipocheza na Aston Villa huko Villa Park
Stephen Keshi amesema kuwa ataendelea kukisimamia kikosi cha soka nchini Nigeria katika mechi ya kuwania taji la ubingwa barani Afrika dhidi ya Sudan licha ya kuwa hajasaini kandarasi mpya.
Mwanamke mmoja nchini Sweden amejifungua mtoto kutokana na kizazi alichowekewa kupitia upasuaji.Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 36 alizaliwa bila kizazi kabla ya kuwekewa kizazi cha mwanamke aliyekuwa katika miaka yake ya sitini.
Viongozi wa Uchina wanasema kuwa maandamano ya kupigania haki ya kuimarisha demokrasia katika eneo la Hong Kong yataambulia patupu.Taariri yenye matamshi makali katika Gazeti la Kikomunisti ilikariri kuwa Serikali inaendelea kumuunga mkono Mkuu wa eneo la Hong Kong, CY Leung.
Mshambuliaji wa kutumainiwa wa Timu ya Simba Hamisi Tambwe leo hasubuhi amefanya mazoezi kwa asilimia 100 na kuondoa uvumi uliokua umemuhusisha kukosa mechi ya kesho dhidi ya stand united
Kampuni ya Microsoft imezindua programu mpya ya Windows 10 ambayo imeipiku Windows 9.Kampuni hiyo pia inatarajia wateja wake watarudi kwani wengi walikuwa wakisitasita kuboresha oparesheni zao tangu Windows 8.
Maafisa wa polisi katikati mwa India wamefutilia mbali harusi kati ya mwanamume mkristo na mwanamke wa kihindu baada ya shinikizo kutoka kwa makundi ya kihindu yenye mrengo wa kulia.
Kuna wakati kila mmoja maishani pengine huhitaji kupata 'hug' (kukumbatiwa) ili kujisikia sio mpweke. Sasa kampuni moja nchini Japan imetengeneza kiti maalum ambacho kitakuwa tayari wakati wowote kumkumbatia na kumliwaza mtumiaji.
Watafiti wamegundua kifaa kipya kinachotumiwa na idadi kubwa ya Sokwe ,Wanasema kuwa kifaa hicho ni ishara tosha kwamba Sokwe wa mwituni wameanzisha tabia mpya.
Kanda ya video inayomuonyesha mtu anayedaiwa kuwa kiongozi wa kundi la Boko Haram imetolewa akikana madai ya jeshi kwamba amefariki.Katika kanda hiyo,Abubakr Shekau anasema kuwa wapiganaji wake waliitungua ndege ya wanajeshi wa angani iliotoweka wiki tatu zilizopita.
Mkufunzi wa kilabu ya Arsenal nchini Uingereza Arsene Wenger amemtaja mshambuliaji wake Danny Welbeck kama mchezaji mwenye kasi ya 'umeme' baada ya kuifungia timu ya Arsenal mabao matatu siku ya jumatano katika mechi ya kilabu bingwa barani Ulaya dhidi ya Galatasaray.