Social Icons

Thursday 2 October 2014

UEFA | Wenger: Welbeck ana kasi ya umeme | Tazama hapa Video ya jinsi alivyofunga magoli 3 Kama hukuona


Mkufunzi wa kilabu ya Arsenal nchini Uingereza Arsene Wenger amemtaja mshambuliaji wake Danny Welbeck kama mchezaji mwenye kasi ya 'umeme' baada ya kuifungia timu ya Arsenal mabao matatu siku ya jumatano katika mechi ya kilabu bingwa barani Ulaya dhidi ya Galatasaray.

Mshambuliaji huyo wa Uingereza mwenye miaka 23 alifunga mabao mawili katika kipindi cha kwanza katika uga wa Emirates kabla ya kupata bao lake la tatu katika kipindi cha pili.
Welbeck sasa amefunga mabao manne katika mechi tatu na Kocha Wenger amesema kuwa alidhani mchezaji huyo ana kasi lakini sasa amebaini kwamba ana kasi ya umeme.




Arsene Wenger

Amesema kuwa ana matumaini kwamba mabao hayo matatu yatampa motisha zaidi.
Danny Welbeck sasa ni mchezaji wa sita nchini Uingereza kufunga mabao matatu katika mechi moja ya kombe la kilabu bingwa barani Ulaya.
Welbeck alicheza kama mshambuliaji mkuu dhidi ya Galatasaray ,huku Alex Sanchez,Mesut Ozil na Alex Oxlade-Chamaberlain wakiwa nyuma yake.
Wanne hao walishirikiana vyema,huku Welbeck akionekana kufanya mashambulizi makali baada ya kupata pasi murua kutoka kwa Sanchez na Oxlade Chamberlain.

MATOKEO MENGINE UEFA JANA
Champions League - Group A October 1
FT Atletico Madrid 1 - 0 Juventus
FT Malmo FF 2 - 0 Olympiakos

Champions League - Group B October 1
FT Basel 1 - 0 Liverpool
FT PFC Ludogorets Razgrad 1 - 2 Real Madrid

Champions League - Group C October 1
FT Zenit St. Petersburg 0 - 0 Monaco
FT Bayer Leverkusen 3 - 1 Benfica

Champions League - Group D October 1
FT Anderlecht 0 - 3 Borussia Dortmund
FT Arsenal 4 - 1 Galatasaray

Tazama hapa>>>>>>

https://www.youtube.com/watch?v=mQd4ho8cFf8

No comments:

Post a Comment