Social Icons

Tuesday 7 July 2015

Yanga Kidume Sakata La Mwashiuya, Kimondo Yakubali Yaishe


Hatimae muvi ya Kimondo na Yanga imefika mwisho baada ya katibu wa Yanga Jonas Tiboroha kufunga safari na kwenda  viunga vya Mbozi kumalizana na Kimondo Sc.



Akizungumza kwa njia ya simu  kutoka Mbozi katibu wa Yanga amesema tatizo lililokuwa kati ya pande hizo mbili limeisha .


“Tumekubaliana mengi na Kimondo fc  mengine hatuwezi kuweka hadharani mojawapo likiwa ni pamoja na kuja kucheza na Kimondo fc na mapato yote kwenda kwa Kimondo fc ikiwa ni sehemu ya shukrani kwa kumkuza Mwashiuya mpaka Yanga tukamuona.”



“Yamesemwa mengi sana na mengi yalikuwa ya uongo na ugovi ukatokea lakini Yanga tumetambua kuwa mwashiuya ni tunda kutoka Kimondo ndio maana tumekuja  lakini nataka kusema kama yanga tukitaka mchezaji huwa hatumkosi kwa vyovyote vile kwa iyo tumemalizana na Kimondo na Mwashiuya ataitumikia Yanga kuanzia leo.”



Kwa upande wa msemaji wa Kimondo fc Chriss Kashililika  naye amekiri kupokea uongozi wa Yanga na kumaliza tatizo hilo.


“Kwa sasa Mwashiuya ni mchezaji halali wa Yanga sisi kama Kimondo tumekubali Yanga wamekubali kuwa Mwashiuya ni mchezaji wa Kimondo ndio maana Yanga wamemtuma katibu mkuu kuja kulimaliza hili .”


Sisi Kimondo tunawajulisha umma kuwa kuanzia leo Mwashiuya ni mchezaji halali wa Yanga baada ya kumalizana na Yanga tumekubaliana mengi ikiwemo na Yanga kuja kucheza mechi Mbozi alikotokea Mwashiuya na Yanga wamekubali watacheza watapokuja kwenye ligi .”


Makubaliano yote yapo kwenye maandishi kama itatokea Kimondo watakuwa nje basi Yanga watakuja kwa mara nyingine lakini pia Yanga wamemuomba radhi mkurugenzi wa kimondo Eliki Ambakisye  kwa yale maneno ya fedheha aliyoongea Jerry Murro.

No comments:

Post a Comment