Social Icons

Monday 6 October 2014

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta Aachia Madaraka Tayari Kutua ICC

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema yuko radhi kwenda katika mahakama ya kimataifa ya ICC kwa kikao maalum kuhusu kesi inayomkabili.
Akiwahutubia wabunge mjini Nairobi,aliwaambia kuwa yuko tayarti kuhudhuria kikao maalum alichotakiwa kuhudhuria mjini Hague bila wasiwasi wowote.
Kenyatta alitakiwa na majaji wa mahakama hiyo kufika ICC tarehe 8 mwezi huu kufafanua madai kuwa serikali yake imekataa kushirikiana na mahakama hiyo hasa upande wa mashitaka kwa kukataa kuipatia ushahidi unaohitajika katika kesi inayomkabili.

Rais Kenyatta anasema anajiamini na kwamba anajua hana hatia katika tuhuma zinazomkabili

Anakabiliwa na tuhuma za kupanga ghasia za kikabila zilizokumba nchi hiyo baada ya uchaguzi wa mwaka 2007/2008.
Aliarifu bunge kuwa anajiamini mwenyewe kiasi cha kuwa tayari kufika mbele ya ICC na kwamba anajua hana hatia katika kesi inayomkabili.
Alisema Kenya ni nchi huru na kwamba haitawahi kuwa chini ya mamlaka nyingine yoyote.

Kenyatta na naibu Rais William Ruto ambaye pia anakabiliwa na kesi katika mahakama ya ICC

Takriban wabunge miamoja wanajiandaa kuambatana na Kenyatta Hague katika ishara yao ya kumuunga mkono.
Uhuru amemkabidhi mamlaka kwa muda naibu wake William Ruto hadi atakaporejea.

No comments:

Post a Comment