Social Icons

Saturday 4 October 2014

LA LIGA | Mabingwa Watetezi Atletico Madrid wapigwa Bao 3 na Vinara wa Ligi, FC Barcelona, washinda Bao 2


LA LIGA Leo hii ilishuhudia Mabingwa Watetezi Atletico Madrid wakipigwa Bao 3-1 na Vinara wa Ligi, FC Barcelona, wakishinda Bao 2-0.Atletico, wakicheza Ugenini, walichapwa na Valencia Bao 3-1 na Wenyeji hao kupata Bao zao zote 3 ndani ya Dakika 13 za kwanza kwa Bao za Joao Miranda, aliejifunga mwenyewe Dakika ya 6, Andre Gomes Dakika ya 7 na lile la Dakika ya 13 la Nicolas Otamendi.

Dakika ya 29 Mario Mandzukic aliipa Atletico Bao lao pekee lakini pia walikosa Penati Dakika ya 45 iliyopigwa na Guilherme Siqueira na wakamaliza Mechi wakiwa Mtu 10 baada ya Alessio Cerci kuzoa Kadi za njano mbili na kuwashwa Kadi Nyekundu.
        XXXXXXXXXXXXX______XXXXXXXXXXXX

FC Barcelona, wakicheza Ugenini na Rayo Vallecano, walishinda Bao 2-0 kwa Bao zilizofungwa ndani ya Dakika moja na Lionel Messi na Neymar katika Dakika za 35 na 36.
Kwenya Mechi hii, Rayo Vallecano walipoteza Wachezaji wawili kwa Kadi Nyekundu katika Dakika za 60 na 90 Jorge Garcia Morcillo na Javier Aquino kutolewa.

LA LIGA
RATIBA/MATOKEO:
Ijumaa Oktoba 3
Getafe CF 1 Cordoba 1
Jumamosi Oktoba 4
Valencia 3 Atletico de Madrid 1
Rayo Vallecano 0 FC Barcelona 2
2100 SD Eibar v Levante
2300 Malaga CF v Granada CF
2300 UD Almeria v Elche CF

Jumapili Oktoba 5
1300 Sevilla FC v Deportivo La Coruna
1800 Celta de Vigo v Villarreal CF
2000 RCD Espanyol v Real Sociedad
2200 Real Madrid CF v Athletic de Bilbao

No comments:

Post a Comment