Social Icons

Saturday 4 October 2014

Louis van Gaal Juan Mata atambadili Nahodha Wayne Rooney Old Trafford Jumapili ,Nahodha Hajulikani


Louis van Gaal amedokeza Juan Mata atambadili Nahodha Wayne Rooney wakati Manchester United inacheza na Everton Uwanjani Old Trafford kwenye Mechi ya Ligi Kuu England lakini alikataa kusema nani atakuwa Kepteni wa Mechi hiyo.

Rooney, mwenye Miaka 28, atazikosa Mechi 3 za Man United baada ya kupewa Kadi Nyekundu kwenye Mechi iliyopita ambayo waliifunga West Ham 2-1.

Van Gaal amedokeza Mata atachukua pozisheni ya Rooney Uwanjani na pia Beki Kinda Paddy McNair, Miaka 19, ambae alicheza Mechi yake ya kwanza kabisa kwa Man United walipocheza na West Ham akiwa Sentahafu, pia atakuwemo Kikosini.

Van Gaal amesema: “Katika nafasi ya Rooney, Juan Mata ameshacheza vizuri sana. Inabidi nichague. Nitamkosa sana Rooney kwa sababu ni Nahodha lakini Mata anacheza vizuri sana nafasi hiyo.”

Kukosekana kwa Rooney Uwanjani kungeweza kumpa utepe wa Unahodha wa Mechi hii na Everton Darren Fletcher ambae ni Makamu wa Nahodha Man United kama atacheza lakini Van Gaal amekataa kuthibitisha hilo.
Van Gaal pia alitoboa kuwa anao Wachezaji 9 wa Timu ya Kwanza ambao ni Majeruhi ingawa wengine washaanza Mazoezi.

Van Gaal ameeleza: “Ni ngumu kueleza. Unaweza ukawa umepona lakini ukawa sio fiti kwa Mechi. Kwa mfano Herrera yuko fiti lakini hatakiwa kuguswa kwenye mbavu. Fellaini amefanya Mazoezi Wiki moja lakini hayuko fiti kucheza Dakika 90.”

Aliongeza: “Tuna Masentahafu watatu majeruhi hivyo MacNair atacheza. Yeye ndio Mchezaji pekee anaeweza kucheza nafasi ya Kulia ya Sentahafu. Nilimchagua Mechi iliyopita na alicheza vizuri sana. Changamoto kubwa kwake ni kumudu kiwango kilekile.”

No comments:

Post a Comment