Social Icons

Sunday 5 October 2014

Sirea A | Juventus Yaendeleza Ubabe Yainyuka 3-2 AS Roma ..Tazama hapa Matokeo Mechi Zote


Mabingwa wa Italy Juventus, wakicheza kwao Juventus Stadium Jijini Turin, Usiku huu wamewabwaga AS Roma ambao walikuwa wamefungana nao kileleni mwa Ligi Serie A Bao 3-2 na kupaa zaidi kileleni.


Kwenye Mechi ambayo iljaa ushindani, bifu Penati mbili na Kadi Nyekundu mbili kwa Mchezaji wa kila upande kutolewa mwishoni, Juve waliibuka kidedea kwa Bao la Beki wao Leonardo Bonucci na kuishushia kipigo chao cha kwa AS Roma Msimu huu.

Mapema Dakika ya 27, Carlos Tevez aliipa Juve Bao la kuongoza kwa Penati na Roma kusawazisha kwa Penati ya Dakika ya 32 iliyopigwa na Francesco Totti kisha Roma kwenda mbele 2-1 kwa Bao la Juan Iturbe Dakika ya 44.

Dakika ya 45, Juve walisawazisha kwa Penati nyingine ya Tevez.

Hadi Mapumziko Juve 2 AS Roma 2.
Bao la ushindi la Juve la Leonardo Bonucci lilifungwa Dakika ya 86 kwa kigongo kikali kufuatia kizaazaa cha Kona.

Dakika mbili baadae kila Timu ilibaki Mtu 10 baada ya Alvaro Morata wa Juve na Costas Manola kuvaana.

Jumamosi Oktoba 4
Hellas Verona FC 1 Cagliari Calcio 0
AC Milan 2 AC Chievo Verona 0
Jumapili Oktoba 5
Empoli          3 U.S. Citta di Palermo 0
SS Lazio 3 US Sassuolo Calcio 2
Parma FC 1 Genoa CFC 2
Udinese Calcio 1 AC Cesena 1
UC Sampdoria 1 Atalanta 0
Juventus FC 3 AS Roma 2
SSC Napoli v Torino FC

SERIE A
Msimamo- Timu za Juu:
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Juventus FC
6
6
0
0
13
2
11
18
2
AS Roma
6
5
0
1
11
4
7
15
3
Sampdoria
6
4
2
0
7
2
5
14
4
Udinese
6
4
1
1
9
5
4
13
5
AC Milan
6
3
2
1
13
9
4
11

No comments:

Post a Comment