Social Icons

Saturday 4 October 2014

BUNDERSLIGA | Borussia Dortmund wameendelea kuwa nyanya Ligi Kuu Ujerumani Msimu huu

Borussia Dortmund wameendelea kuwa nyanya kwenye Bundesliga Msimu huu baada kuchapwa 1-0 wakiwa Uwanjani kwao Signal Iduna Park na SV Hamburg.Hii ni Mechi ya 4 sasa ya Ligi ambayo Dortmund hawajaonja ushindi na Bao la Leo lililowamaliza lilifungwa na Pierre-Michel Lasogga katika Dakika ya 35.

Lakini Mabingwa Watetezi Bayern Munich, wakiwa kwao Allianz Arena, waliichapa Hannover Bao 4-0.
Bao za Bayern zilifungwa na Robert Lewandoski na Arjen Robben, kila mmoja akipiga Bao 2.

Ushindi huu umewabakisha Bayern kileleni wakiwa na Pointi 17 wakifuatiwa na Hoffenheim wenye Pointi 13 na Dortmund ipo Nafasi ya 13 ikiwa na Pointi 7.

RATIBA/MATOKEO:
Ijumaa Oktoba 3
Hertha Berlin 3 VfB Stuttgart 2

Jumamosi Oktoba 4
Bayer 04 Leverkusen 2 SC Paderborn 2
Bayern Munich 4 Hannover 0
BV Borussia Dortmund 0 Hamburger SV 1
SV Werder Bremen 1 SC Freiburg 1
TSG Hoffenheim 2 Schalke 1
1930 Eintracht Frankfurt v FC Koln

Jumapili Oktoba 5
1630 VfL Wolfsburg v FC Augsburg
1830 Borussia Mönchengladbach  v FSV Mainz 05

No comments:

Post a Comment