Social Icons

Monday 18 January 2016

Tazama Ratiba na Matokeo Ya Michuano Ya CHAN 2016 Huko Rwanda


Huko Rwanda, kwenye Fainali za 2016 African Nations Championship (Chan 2016), ambazo ni  Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wachezao ndani ya Afrika zilizoanza Jumamosi, Tunisia na Guinea zilitoka 2-2 wakati Nigeria ikiibonda Niger 4-1 kwenye Mechi za Kundi C zilizochezwa Stade Régional de Nyamirambo.



 
Bao za Tunisia zote zilipachikwa na Ahmed Akaichi, Dakika 33 na 51, wakati zile za Guinea zikifungwa na Alseny Camara katika Dakika za 40 na 83.
Kwenye Mechi ya Nigeria na Niger, Osas Okoro aliipa Nigeria Bao la kwanza Dakika ya 46 na kisha Chisom Chikatara akapiga Hetitriki kwa Bao za Dakika za 75, 82 na 90 huku Bao pekee la Niger likifungwa Dakika ya 81 na Adebayor Zakari Adje.

RATIBA NA MATOKEO

Jumatatu Januari 18
Tunisia 2 Guinea 2 
Nigeria 4 Niger 1     
Jumanne Januari 19
Zimbabwe v   Zambia Rubavu 16:00       
Mali v  Uganda Rubavu 19:00       
Jumatano Januari 20
Rwanda v Gabon Amahoro, Kigali 16:00
Morocco v Ivory Coast Amahoro, Kigali 19:00   

No comments:

Post a Comment