Social Icons

Tuesday 19 January 2016

Tetesi Za Usajili Ulaya Jan 19 , Van Gaal Out , Lukaku , Ighalo , Tiote , Berahino Wanaelekea Huku



Kocha wa Mashetani wekundu wa Jiji la Manchester ,Manchester United Louis Van Gaal Mkataba wake unamalizika mwaka 2017 lakini inaonekana kuwa hataweza kuumaliza mkataba huo akiwa ndani ya United na Sio Chaguo sahihi la Red Devils.


Kwa Mujibu wa Jarida la The Mirror Mdachi huyo anajiandaa kuachana na timu hiyo Msimu huu kutokana na Pressure Kubwa anayoipata ndani ya Old Trafford nay eye kama meneja hajawa na furaha kutokana na hali ya klabu na ataacha na timu hiyo huku akisaliwa na mwaka mmoja kwenye mkataba wake na huwenda United wakamvunjua mkataba na kumlipa stahiki zake.

Endapo Van Gaal ataachia ngazi Mwenyewe Klabuni hapo Kunataarifa kuwa aliyekuwa Meneja wa Chelsea Mreno Jose Morinho ndiye atakayechukua Pahala Pake, Ryan Giggs ambaye ni meneja msaidizi hawezi kuiongoza United kama Kocha Mkuu.


Everton Man United Mtupe £65m kwaajili ya Lukaku

Klabu ya Everton imewaambia Manchester United Kuwa Wanapaswa Kulipa Kitita cha £65 million kama wanahitaji Saini Ya Mshambuliaji wa Timu Hiyo Mbelgiji Romelu Rukaku.


Kwa Mujibu wa The Sun Lukaku anatazamwa kwa Ukaribu sana na Vilabu vya Real Madrid, Paris Saint-German na Manchester City Pamoja na Manchester United na Everton Wanafanya Kila Wawezalo Kumbakiza Mchezaji huyo Goodson Park kwa Kutaja dau kubwa kwa vilabu vinavyo Muhitaji Lukaku, Mpaka sasa Lukaku anamkataba wa miaka mitatu na nusu ndani ya Everton.


Wakati huo huo Klabu ya Chelsea bado inania ya kumsajili beki kisiki wa Everton John Stone Japo Kuwa Bado Klabu yake inasisitiza kuwa Nchezaji huyo hauzwi .


Newcastle Kufanya Usajiri wa  Berahino na Townsend


Newcastle United bado wanajaribu kutaka kufanya Usajili wa Wachezaji wawili Saido Berahino na Andros Townsend, Wachezaji hao wa West Brom na Tottenham watapeleka utofauti ndani ya NewCastle lakini bado wanaendelea kufanya mazungumza ili kuzinasa saini za nyota hao,

Spurs tayari wanaonekana kutaka kukubali kumuachia Townsend kwa Mkopo na baadaye kumuachia moja kwa moja mchezaji huyo huku wakiendelea kujadili dili la £14m kwaajili ya winga huyo huku Newcastle wanaamini kuwa watampata mchezaji huyo kwa mkopo na watamnunua moja kwa moja endapo atafanya vizuri ndani ya Newcastle.

Chelsea Kumnasa Mshambuliaji Ighalo


Klabu ya Chelsea hivi sasa wanatazama Watford kwaaji ya kumpata Mshambuliaji Mpya. The Blues wamekuwa wakimfwatilia kwa ukaribu Odion Ighalo na wanaamini  kuwa watafanya usajili wa Mnigeria huyo Msimu huu. 

Kwa Sasa Chelsea  wanaorodha ya Washambuliaji ambao hawana muda mrefu wakuendelea kukaa Stamford Bridge kwa Msimu huu Radamel Falcao na Loic Remy Wataondoka Klabuni hapo Msimu ujao, the Blues wanahitaji kuwa na Mshambuliaji wa muda mrefu na  Ighalo anaonekana kuwa mrithi sahihi wa wachezaji hao na Chelsea wapo tayari kufanya usajiri wa mchezaji huyo. 

Lakini Pia Kunataarifa kuwa Arsenal nao wanamuwania mshambuliaji huyo wa Watford ili akaisaidie timu hiyo hasa kumaliza tatizo la Ushambuliaji Emirate.

Tiote Safari ya China Imekufa



Cheick Tiote  hata Ondoka NewCastle United Kuelekea China ambako alikuwa anahusishwa na kujiunga na klabu ya Shanghai Shenhua na dili hilo limekufa kwakuwa Tiote huwenda akaongezewa mshahara wa £60,000 kwa Wiki baada ya Makato na Mazungumzo yanataraji kuanza hivi punde .

Newcastle na Shanghai walikubaliana kiasi cha £8m kwaajili ya Tiote kama Ada ya Uhamisho ili akafanyiwe Vipimo vya Afya lakini Klabu hiyo ya China Inaona kuwa bado Pesa hiyo Ninyingi na Kocha Steve MacClaren anataka Kutumia Pesa Hiyo Kwaajili yak ukitengeneza kikosi Chake Upya

No comments:

Post a Comment