Social Icons

Saturday 28 June 2014

Kombe La Dunia Penalti Zaiokoa Brazil , Rodriguez Awaadhibu Uruguay Colombia Robo Fainali Kucheza na Brazil


Kocha wa Brazil Luiz Felipe Scolari amesema Timu yake imebakisha Gemu 3 kufika ’Peponi’ baada Jana kuibwaga Chile kwa Mikwaju ya Penati 3-2 baada ya Sare ya Bao 1-1 katika Dakika 120 za Mchezo za Mechi ya Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia.




Kwenye Robo Fainali, Brazil watacheza na Colombia ambao Jana waliwafunga Uruguay 2-0.Scolari amesema: “Tuliazimia wenyewe kwenye dhima hii tuwe Mabingwa. Ukiweka ahadi ni lazima uitimize. Hili ndio Wachezaji wanafanya!”
Aliongeza: “Bado zipo Gemu 3 zaidi na tutaona kama tutafika peponi!”
Kabla ya Mechi na Chile, Scolari alikiri kucheza na Chile ni ‘maumivu’ na pia kubaini Wachezaji wake kidogo wana mchecheto.

Scolari, ambae aliiongoza Brazil kutwaa Kombe la Dunia Mwaka 2002, alisema: “Kila Mechi inazidi kuwa ngumu na ugumu unaongezeka! Kombe la Dunia limeonyesha Timu zinalingana. Kama hutumii nafasi moja au mbili unazopata, kama tulivyofanya Leo, basi unaweza kuadhirika na kutolewa.”

KOMBE LA DUNIA: COLOMBIA YAIPIGA URUGUAY, ROBO FAINALI KUIVAA BRAZIL! 

James Rodriguez, Kijana wa Miaka 22 anaechezea AS Monaco ya Ufaransa, Jana alifunga Bao 2 na kuipeleka Colombia, kwa mara ya kwanza katika Historia yao, Robo Fainali ya Kombe la Dunia baada Colombia kufunga Uruguay Bao 2-0 Estadio Maracana Jijini Rio de Janeiro Nchini Brazil.

James Rodriguez pia ameweka Rekodi ya kuwa Mchezaji wa kwanza tangu Ronaldo wa Brazil Mwaka 2002 kufunga Bao katika kila Mechi katika Mechi zake 4 za kwanza za Fainali za Kombe la Dunia.

Uruguay, wakicheza bila Staa wao Luis Suarez aliefungishwa virago na FIFA kwa kufungiwa Miezi Minne kwa kumng’ata Beki wa Italy Giorgio Chiellini, walizidiwa maarifa na Timu ya Ciolombia Kwenye Robo Fainali, Colombia watacheza na Wenyezi Brazil hapo Ijumaa Julai 4 huko Estadio Estadio Castelão, Fortaleza.

No comments:

Post a Comment