Social Icons

Sunday, 20 October 2013

Roma yaendeleza ushindi Seria A.

Klabu ya Roma imeendeleza wimbi lake la ushindi kwa mechi ya nane mfululizo mara baada ya kuifunga Napoli goli 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Ya Italia”Seria A” Ijumaa Usiku.

Kiungo raia wa Bosnia,Miralem Pjanic ndiye aliyeizamisha Napoli inayonolewa na Benitez kwa kupachika magoli yote mawili na kuwa kipigo cha kwanza kwa kocha huyo Muhispania katika Ligi hiyo.
Vijana hao Rudi Garcia walicheza kwa juhudi sana mchezo huo wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Stadio Olimpico.Huku wakiwa na rekodi nzuri ya kuruhusu nyavu zao zitikiswe mara moja tu mpaka sasa.
Pia mchezaji wa Napoli,Paolo Cannavaro alitolewa nje kwa kadi nyekundu mara baada ya kupewa njano ya pili katika dakika ya 70 akicheza faulo iliyozaa penati.
Kwa matokeo hayo Roma wanaendelea kuwa kileleni wakiwa na pointi 24 mara baada ya kushinda michezo yote nane huku Napoli ikifuatiwa katika nafasi ya pili kwa pointi 19.

No comments:

Post a Comment