MENEJA wa zamani wa klabu
ya Manchester United, Sir Alex Ferguson ametuma ujumbe wa onyo kwa
mrithi wake David Moyes kuwa siri kubwa ya mafanikio Old Traford ni
umoja na maelewano haswa katika vipindi vigumu.
Kwasasa United inashika nafasi ya tisa katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza, ukiwa ni mwanzo mbaya zaidi kwa timu hiyo katika miaka 20 iliyopita.
Akizungumza katika semina na mafundisho ya ukocha huandaliwa na Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA, Ferguson amesema kuna vitu vitatu vya msingi wakati unafanya kazi na benchi lako la ufundi ambavyo ni maadili ya kazi, uaminifu na falsafa. Ferguson amesema ni muhimu watu wako wakakubaliana na wewe na unavyotaka na njia unazotaka klabu yako icheze. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa ilikuwa ni vigumu zaidi kufanya kazi na watu miaka 30 iliyopita tofauti na sasa ambapo watu wengi aliokuwa nao walikuwa ni waelewa na wanaotoka katika mazingira mazuri.
No comments:
Post a Comment