Social Icons

Sunday, 20 October 2013

Flamini kitendawili Ligi ya Mabingwa.

Kocha wa Arsenal,Arsene Wenger amesisitiza kuwa kiungo wake,Mathieu Flamini yupo kwenye hatihati kubwa ya kukosa mchezo wa Ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Borussia Dortmund wiki ijayo.

Flamini alipata jeraha la mshtuko wa ubongo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza walipoifunga Norwich City 4-1 na kulazimika kutolewa katika kipindi cha kwanza.
Wenger anasubiri taarifa ya mwisho kutoka kwa madaktari ili kuthibitisha rasmi ukubwa wa tatizo kabla hajatangaza kikosi kitakachohusika katika mchezo dhidi ya Dortmund siku ya Jumanne katika uwanja wa Emirates.
Mfaransa huyo alisema kuwa anasubiri ushauri wa daktari ingawa anafahamu kuwa kupata tatizo kama hilo huwa inatakiwa mchezaji akae nje kwa siku tano.Pia akadai kuwa alimtoa nje kiungo huyo mkabaji kwasababu hakutaka apate matatizo makubwa zaidi.

No comments:

Post a Comment