Messi mwenye umri wa miaka 26 alikosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Celtic ambao Barcelona ilishinda kwa bao 1-0
na mechi nyingine ya La Liga dhidi ya Villadolid ambao nao walishinda kwa mabao 4-1 ikiwa ni matokeo ya majeraha hayo aliyopata mwezi uliopita. Nyota huyo ambaye tayari ametupia mabao nane katika mechi sita alizocheza ameonyesha kupona majeraha yake ingawa haijajulikana kama atacheza katika mechi ya La Liga kati ya Barcelona na Osasuna Jumamosi ijayo. Baada ya mechi hiyo dhidi ya Osasuna,
Barcelona itakuwa inakabiliwa na michezo miwili muhimu mmoja ukiwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya AC Milan na mwingine wa La Liga dhidi ya mahasimu wao Real Madrid.
No comments:
Post a Comment