Social Icons

Friday, 18 October 2013

Iraq yanunua silaha za mabilioni ya dola kwa Russia

Russia imeanza kusafirisha silaha kuelekea Iraq chini ya makubaliano ya kihistoria ya ununuzi wa silaha za mabilioni ya dola yaliyofikiwa kati ya pande mbili mwaka uliopita. Ali al Musawi mshauri wa masuala ya habari wa Waziri Mkuu wa Iraq Nour al Maliki amesema,
mkataba huo unajumuisha ununuzi wa silaha ndogo ndogo kwa ajili ya kukabiliana na ugaidi.  Baghdad na Moscow zilisaini mkataba wa dola bilioni 4.3 mwezi Oktoba mwaka uliopita, na kuifanya Russia kuwa muuzaji mkubwa wa pili wa silaha wa Iraq baada ya Marekani. Hata hivyo makubaliano hayo hayakutekelezwa haraka kutokana na hofu ya ufisadi.
Iraq pia imeeleza kuwa haina nia ya kuwa na silaha za mashambulizi na kwamba zana hizo ni kwa ajili tu ya kuimarisha usalama wa nchi, kulinda utajiri wake na kupambana na ugaidi.

No comments:

Post a Comment