Afisa wa ngazi za juu wa Kongo
Brazaville amesema kuwa, wanajeshi wa Angola wamevuka mpaka na kuingia
katika ardhi za nchi hiyo jirani mapema wiki hii na kukamata kikundi cha
askari wa Kongo. Kanali Christian Sansa kamanda wa jeshi la Kongo
Brazaville amesema kuwa, wanajeshi wa Angola waliingia katika wilaya ya
Kimongo kutokea Cabinda na kudai kwamba walikuwa katika ardhi yao.
Sansa
ameongeza kuwa Kongo imepeleka askari wake kwenye eneo hilo baada ya
kufahamu suala hilo lakini walishikiliwa na wanajeshi wa Angola. Hata
hivyo balozi wa Angola mjini Brazzaville amesema kuwa hana taarifa juu
ya harakati za askari wa Angola ndani ya ardhi ya Kongo na kukanusha
kushikiliwa askari wa Kongo Brazaville na wanajeshi wa nchi yake.
Suala hilo linaashiria wasiwasi uliopo
katika eneo la Cabinda la Angola lenye utajiri wa mafuta lililojitenga
na nchi hiyo na linalopakana na Kongo DRC na Kongo Brazaville.
No comments:
Post a Comment