Mabingwa watetezi wa ligi hiyo maarufu kama La Liga,Barcelona wakiwa bila ya Lionel Messi ambaye bado majeruhi walitoka sare ya 0-0 katika mchezo mgumu ikiwa ni mechi yao ya kwanza kutopata pointi zote tatu mara baada ya kushinda mfululizo tangu ligi hiyo ianze.
Atletico Madrid ikapokea kipigo kwa mara ya kwanza cha goli 1-0 wakiwa wageni wa Espanyol na kuharibiwa rekodi yao ya kushinda mfululizo tangu ligi imeanza kama wenzao Barcelona.
Kwa matokeo hayo Barcelona wanaendelea kuwa kileleni mwa msimamo kwa kufikisha pointi 25 huku Atletico Madrid ikiwa bado nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 24,timu zote zikiwa zimeshuka dimbani mara tisa.
No comments:
Post a Comment